JE HUYU NI KIONGOZI KIJANA MFANO WA KUIGWA TANZANIA KWASASA?Inawezekana ukafikiri kwamba ni ngumu kwa viongozi wetu wa nchi kuwatia moyo wananchi wao kwakutumia vifungu mbalimbali vya Biblia ama kwakutumia imani yao. Basi hii si mara ya kwanza kuandika kuhusiana na mkuu wa wilaya bwana Mrisho Gambo (mkuu wa wilaya ya Uvinza Kigoma) wakati huo tulipoandika alikuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe, Tanga.

Ni kwamba licha ya uchapakazi wake hodari katika kuleta maendeleo mahali anapopangiwa kazi zake na kutoa taarifa za kazi mbalimbali zinazoendelea katika wilaya yake kupitia mitandao ya kijamii hususani Facebook na Instagram. Mkuu huyu amekuwa akitoa maneno mengi ya kutia moyo watu  na kubariki waliowengi. Moja ya maneno aliyotoa wiki iliyoisha na kupata wapenzi wengi waliopenda ujumbe wake ni huu hapo chini ambao watu zaidi ya 400 pia walishare kwenye kurasa zao, sambamba na baadhi ya jumbe nyingine alizowahi kutoa kwa mwezi May.  Mrisho ni mume wa mke  mmoja na watoto wawili 

Ndugu Mrisho Gambo,  GK inakutakia utumishi mwema uliotukuka, Mungu awe kiongozi wako na mlinzi wako daima akutimizie haja ya moyo wako, sawasawa na mapenzi yake juu ya maisha yako


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.