KIJANA AJITOSA KATIKATI YA SIMBA AKIDAI KAAGIZWA NA MUNGU

Franco akiwa amebanwa kabla ya kuokolewa. ©Daily Mail
Kwa wafuatiliaji wa somo la namna ya kuisikia sauti ya Mungu kwa urahisi zaidi, hawatokuwa na mashaka kwamba kijana huyu alisikia ndivyo sivyo, maana kwa maelezo yake anadai kwamba amesikia sauti ikimtuma kuingia humo ndani ya uzio wa simba. Kufanya nini? Hajaeleza zaidi, lakini tarehe 21 Mei ndio siku aliyochagua kufa. Japo haikuwezekana.

Siku ya tukio nchini Chile, kijana Franco Luis Ferada Roman aliamua kutembelea eneo lililohifadhiwa wanyama, (Zoo) , na kulipia kiingilio kama watu wengine waliojitokeza. Lakini ndani yake akili ilikwishaamua, ya kwamba ni lazima aingie ndani akakutane na simba, na kana kwamba hakutaka simba wahangaike kuzichambua nguo kabla ya kumtana, alimua kuweza nguo zake kando na kisha akatumia njia ya paa kuingia ndani ya boma hilo la simba.

Taharuki ilianzia papohapo kwa watazamaji waliotembelea eneo hilo, kuona kijana akiwa kando ya simba kama alivyozaliwa, na kisha wale simba wakaanza kumzonga zonga, lakini wakicheza naye kwanza.

Kelele za nje  na pengine hofu iliyotibuliwa ndiyo ilipelekea simba nao kumaliza mchezo wao baada ya kushindwa kujua nia ya Franco ni nini, na hivyo kuanza kumpelekesha, jambo lililofanya Franco aanze kupiga kelele na kulitaja jina la Yesu.

Isingekuwa kwa walinzi wa eneo hilo ambao walilazimika kuwaua simba wawili kati ya watatu waliokuwemo humo ndani kwa risasi, basi huenda Franco angeshakuwa amechongewa jeneza sawasawa na urefu wake. Madaktari wanaomtibu wameeleza kwamba pamoja na kwamba alikuwa mahututi, kwa sasa anaendelea vema baada ya kupata matibabu. Hatua inayofuata inaelezwa ni kumpima akili yake baada ya kuonekana akitaka kujaribu kama ambavyo Sura ya 6 ya Kitabu cha Danieli inavyoeleza namna Danieli alivyokuwa na simba bila madhara yoyote. Naye akadhani huenda wale simba watakuwa kama paka wake wa nyumbani.

Baba mzazi wa Franco ameoneshwa kushtushwa na tukio hilo, ambalo hajui mwanzo wake ulikuwajekuwaje. Huku wazazi waliokuja na watoto wao wakisikitikia kitendo hicho, ambapo walichoweza kufanya ni kuwaziba watoto macho yao ili wasishuhudie mtu akifa kikatili.

Hata hivyo kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari nchini Chile, inaelezwa kwamba mwisho wa dunia ni sababu mojawapo ya kijana huyo kutaka kuyamaliza maisha yake, kulingana na ujumbe waliokuta amendika.

Bofya hapa kujifunza; Namna ya Kuisikia Sauti ya Mungu kwa Urahisi Zaidi.
Sehemu ya Kwanza | Sehemu ya pili | Sehemu ya tatu | Sehemu ya nne


Vyanzo:
International Business Times | Chile Television

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.