KUTOKA JUMBA LA WASHINDI: PASIPO MAONO, HAKUNA UELEKEO - SHEMEJI

Kama umekuwa mbali na tukio la leo, basi Gospel Kitaa inakuletea kwa uchache yaliyojiri. Tunaanza na Mwalimu Shemeji Melayeki, ambaye amegusia kuhusiana na maono.


Dondoo kadhaa ni kama zifuatazo;

Maono yemetokana na tatizo, pale unapoona jambo linaenda kombo mtaani kwako, basi wewe ndiye unayetakiwa kutafuta suluhu. maono yapo japo upate kutengeneza.

Mtu akikukuta unawaza kusolve matatizo ya watu, hawezi kukudharau. Lakini iwapo hutokuwa ukifanya jambo lolote, basi hutokuwa tofauti na wale wasio na maono.

Vitu ambavyo watu wamevikatia tamaa, tuna uwezo wa kutengeneza kama voijana, maana uwezo tumepewa na Mungu. Wanaposema jmbo fulani haliwezekani, basi ndio fursa kwako, maana hakuna lisilowezekana kwa kila aaminiye.

Umaarufu ni matokeo ya mtu ambaye yuko makini na jambo alifanyalo. Cha muhimu ni kuendelea kutibu matatizo ya jamii, hapo kuonekana kupo.

Unawezaje kutambua maono uliyonayo kama kijana? Tukutane kesho Jumapili hapahapa Jumba la Washindi, Victory Faith, Kijenge Jijini Arusha.Hii ndio #Inspired4Change. Picha kamili za tukio zitakujia baadae. Tukutane Jumapili kuanzia saa nane mchana.


Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.