MAMA YAKE ALITAKA KUUTOA UJAUZITO WAKE KWASABABU YA UMASKINI LAKINI SASA NI MWANASOKA NYOTABrazil ni moja kati ya mataifa ambayo wananchi wake wanamwabudu Mungu sana lakini pia likiwa katika matatizo mengi yakiwemo masuala mazima ya mapenzi ya jinsia moja. Uhakika wa taifa hili kumpenda Mungu linaweza kuonekana kupitia wachezaji mpira maarufu wa timu hiyo ambayo imebeba kombe la dunia mara kadhaa, kati ya wachezaji hao ni pamoja na Kaka, ambao kwasasa wamestaafu lakini leo nataka nikujulishe japo kwa ufupi kuhusu mchezaji Thiago Silva anayekipiga barani Ulaya na timu ya Paris Saint Germaine (PSG).

Kikubwa usichofahamu kuhusu mchezaji huyu ni kwamba Mungu ni kimbilio la maisha yake, katika mambo yote anayoyafanya amesema amekuwa akimtanguliza Mungu hasa ukizingatia kwamba kwa hali aliyopitia hakutakiwa kuwa hai mpaka leo lakini ni rehema za Mungu zilizomuweka hai mpaka sasa. Wakati wa ujauzito wa mchezaji huyu mama yake aitwaye Angela alitakiwa kutoa ujauzito wake kwakuwa hakuwa na uwezo wa kumlea mtoto endapo atazaliwa mawazo ambayo alikuwa akipingana nayo lakini mama huyo anasema hiyo ndiyo ilikuwa hali halisi kwakuwa hakuwa na uwezo wa kuwa na mtoto mwingine kutokana na umaskini uliokithiri

Hata hivyo ni babu yake na mchezaji huyo alimtia moyo binti yake kutoutoa ujauzito huo kwakuwa
ni dhambi kubwa kufanya hivyo. Hata Thiago alivyozaliwa alianza safari ya matatizo kwa kuugua kifua kikuu alipokuwa na miaka 14 ugonjwa uliomfanya akae hospitali kwa miezi 6 mpaka alipopona. Mchezaji huyo aliyetokea katika kitongoji cha Shantytown jirani na jijini Rio de Janeiro, amesema ni mono wa Mungu tu ndio uliomlinda mpaka kuwa mchezaji wa kimataifa kwakuwa katika kitongoji chake kulikuwa na uhalifu mkubwa uliopelekea milio ya risasi kila leo, na polisi walikuwa wakija kila kukicha hali iliyofikia kusema kwamba endapo akitoka na kurudi salama nyumbani alimshukuru Mungu.

Anasema licha ya hali halisi iliyokuwa ikiendelea katika kitongoji chao ilikuwa rahisi kwake kujikita kwenye uhalifu lakini aliamua kumchagua Mungu kuwa kiongozi wake na hatimaye kufanikiwa kufikia malengo yake ya kuwa mchezaji wa kimataifa. Thiago amesema maisha ya soka hayakuwa rahisi kwake kwani hakuweza kuchaguliwa kwenye timu ya kwenye kitongoji chake na kuishia kuchezea timu za mchangani, lakini juhudi, nidhamu na kumtanguliza Mungu mbele kufeli kwake kukageuka mafanikio kwakupata kuonekana barani Ulaya baada ya kupata mkataba na klabu ya Urusi na matokeo yake akapata mkataba na PSG ambako analipwa dola za kimarekani milioni 16 kwa mwaka.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.