MSHINDI WA UREMBO MISS USA ABADILI DINI YA KIISLAMU NA KUMFUATA KRISTO

Rima Fakih ©RimaFakih

Mlimbwende aliyewahi kushinda shindano la urembo la Miss USA 2010 akiwa muumini wa kwanza wa kiislamu kushiriki mashindano hayo nchini Marekani aitwaye Rima Fakih ameamua kubadili dini na kumfuata Kristo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Kingdomboiz umedai kwamba mrembo huyo alikata shauri na kumfuata Kristo mwezi uliopita ikiwa katika maandalizi ya kuolewa na mtayarishaji muziki wa injili tajiri aitwaye Wassim Salibi katika ndoa wanayotarajia kufunga huko nchini Lebanon wiki ijayo

 
Aliposhinda shindano hilo alikiri kwamba aliamua kuwa muislamu wakati alipoanza chuo, alikaririwa akisema "Ningependa kusema, mimi kwanza ni Mmarekani, nimetokea Lebanon (mimi ni mmarekani mwenye asili ya kiarabu) pia ni muislamu mmarekani". Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa habari wa Albawaba, Fakih alijiunga na asili ya dini yake alipojiunga chuo.

Mrembo huyo akaongeza kwamba alipojiunga chuo kikuu cha Michigan kwasababu kulikuwa na waislamu wengi, baba yake akamtaka kujifunza dini ya kiislamu kwa kujiunga na jumuiya ya kiislamu, amedai kwamba hakujua kuhusu mwezi wa ramadhani na sikukuu nyingine za dini yake na kwamba baba yake akamtaka kutumia nafasi hiyo kujifunza.

Aidha mrembo huyo amekuwa akitumia mtandao wake wa twitter kuandika jumbe mbalimbali kutoka kwenye Biblia kama picha zinavyoonyesha.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.