MWINJILISTI ALIYEHARIBIWA KWA TINDIKALI BAADA YA KUHAMA UISLAMU, AMSHUKURU MUNGU KWA UPONYAJI

Mwinjilisti Umar Mulinde picha wakati akipatiwa matibabu miaka 2 iliyopita©Mulinde

Ikiwa takribani miaka mitano ipite tangu mwinjilisti Umar Mulinde kujeruhiwa vibaya kwa kuharibiwa mwili kwa tindikali aliyomwagiwa na watu wanaosadikiwa kuwa waumini wa dini ya kiislamu waliokuwa wakipinga hatua yake ya kubadili dini na kuwa Mkristo, hapo juzi mwinjilisti huyo alifanya ibada maalumu ya shukrani kukumbuka namna tukio hilo lilivyotokea na kumuharibu kabisa sura yake yenye mvuto.

Katika jumble wake kupitia okras wake wa Facebook mwinjilisti huyo aliandika namna ambavyo kupitia nguvu ya maombi na neema ya Mungu ilivyomponya katika tukio hilo la kuogofya, bila kusahau kutaja madaktari waliomuhudumia huko nchini Israel ambako alihamishiwa kupata matibabu yaliyokwenda sambamba angalau kurudisha sura yake kwenye muonekano mzuri.

Mwinjilisti Umar Mulinde raia wa Uganda ambaye baba yake ni imamu wa msikiti nchini humo, alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa na imani kali ya uislamu na hata kufikia hatua ya kuwachukia kupita kiasi waumini wa dini ya Kikristo likiwemo taifa la Israel, hata hivyo mambo yalibadilika baada ya kukutana na Yesu ambaye alimbadilisha maisha yake ambapo aliapa kutorudi nyuma kamwe licha ya tukio hilo kubwa na vitisho anavyopata kutoka kwa waumini wa dini aliyokuwepo awali.

Unaweza kutazama na kusoma zaidi habari za mwinjilisti huyu kuanzia alipomwagiwa tindikali mpaka hali aliyonayo sasa kwa Kubonyeza HAPA.Chini ni ujumbe alioundika mwinjilisti huyo kupitia katika ukurasa wake kwa undani zaidi 


Mwinjilisti Mulinde alivyokwasasa.
Yesterday 17/5/2016, was a wonderful PRAISE & Thanksgiving Day as many joined in to remember how I was targeted in a horrific Acid attack, the way God saved me with his grace, power, prayers of many sympathizers around the world and the expertise of Israel Doctors!
When acid is thrown on a person, the result is horrifying; it causes the skin tissue to melt, often exposing the bones below the flesh, sometimes even dissolving the bones.
An acid attack on your body would dramatically change your life.
In Uganda, Acid has killed many people because Nitric, hydrochloric, or sulfuric acids all have a catastrophic effect on human flesh.
Defying all that and coming back to meaningful service is a matter that deserves Praise and thanksgiving to God – Halleluiah.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.