MZAZI WA MWIMBAJI WA KWETU PAZURI AFARIKI DUNIA, MAZISHI KUFANYIKA LEO

Steven Gakwaya mtoto wa marehemu
Mmoja wa waimbaji wakongwe wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda almaarufu kama "Kwetu Pazuri" ajulikanaye kwa jina la Steven Gakwaya akifahamika zaidi kwa jina la Sunday hapo juzi jumamosi baba yake alitwaliwa kutoka katika ulimwengu huu. Taarifa za kufariki kwa mzazi wa mwimbaji huyo zimetolewa na kundi hilo wakisema mzee wao (ambaye ni mzee kiumri) aliugua kwa muda mrefu pamoja na matatizo mbalimbali ya kimaisha na hatimaye mauti ikampata hapo jana.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba kawa hiyo imehudhuria mara kadhaa katika kumjulia hali mzee huyo na kumtia nguvu mwimbaji mwenzao wakati wa kuuguza, lakini pia ni kwamba walifahamu kwamba tukio hilo litatokea na kumtaka mwimbaji mwenzao kujipa moyo na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya wokovu waliyotupatia, pia waliweka vifungu mbalimbali vya biblia katika kusindikiza maneno yao.  Mazishi ya mzee huyo yanatazamiwa kufanyika hii leo nchini humo.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana Libarikiwe.

Marehemu Mzee Gakwaya enzi za uhai wake

Mzee Gakwaya wakati wa ugonjwa ©AOC
             Farijika na wimbo huu kutoka album zilizopita za AOC "Mtegemee Yesu"Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.