NYOTA WA INJILI TANZANIA AENDELEA KUFANYIKA BARAKA NCHINI MAREKANI

Upendo JBride
Mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini mwanamama Upendo JBride Mwakyegula ambaye kwasasa ni ametunukiwa udaktari kutokana na huduma yake, amezidi kufanyika baraka huko nchini Marekani ambako anafanya ziara ya kihuduma.

Jumapili ya iliyoisha mwanamama huyo ambaye uwezo wake wa kucheza na sauti na nyimbo nyingi zenye upako aliweza kuwasimamisha watoto, vijana kwa wazee katika kumsifu Mungu pale alipofanya huduma katika kanisa la Harvest Center International lililopo katika kitongoji cha Wilmington huko Delaware Marekani. Kupitia ukurasa wao wa Facebook wa kanisa hilo waliweza kuelezea vyema namna mwanamama huyo alivyofanyika baraka kwa huduma yake. Ili kujisomea unaweza kubonyeza HAPA.

Aidha mwimbaji huyo ambaye ziara yake itachukua jumla ya miezi mitatu kabla ya kurejea nchini, yupo mbioni kuachia album mpya yenye vionjo mbalimbali ambavyo kwa baadhi yake GK imepata fursa ya kusikiliza. Habari zaidi kuhusu mwinjilisti huyu Dkt Upendo JBride endelea kutembelea Gospel Kitaa (GK).                     Jikumbushe moja ya nyimbo zilizopita kutoka kwa Upendo JBride


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.