PATA MBINU MPYA YA UFUNDISHAJI WANAKWAYA KAMA HUIJUI

Mwalimu kiongozi wa BTC Mrs Carol Cymbala akiwa mazoezini na waimbaji ambao walitumika kuwafundisha wenzao ©BTC

Yawezekana kuna baadhi ya vikundi ambavyo vilishaanzisha namna hii ya ufundishaji au bado, ni kwamba kwaya maarufu na kongwe duniani ya The Brooklyn Tabernacle ya jijini New York nchini Marekani wiki iliyoisha iliweza kuweka wazi moja ya mbinu za ufundishaji wa nyimbo kwa wanakwaya wake.

Kwaya hiyo ambayo ina waimbaji zaidi ya 300 wakiwa washindi wa tuzo 6 za Grammy, chini ya mwalimu wao mkuu ambaye ni mke wa mchungaji kiongozi na mwanzilishi wa kanisa hilo Carol Cymbala aliyeisimamia kwaya hiyo kwa miaka 40 sasa. Kwasasa endapo wananyimbo mpya huwafundisha baadhi ya waimbaji kutoka kila sauti kisha wanasimama mbele ya wanakwaya wenzao na kuimba huku wenzao wakipata nafasi ya kushika sauti zao na kuimba.

The Brooklyn walitoa picha wiki iliyopita kwenye ukurasa wao wa Facebook na kuandika kichwa cha habari namna mpya ya kufundisha waimbaji kwa kusikia kutoka kwa wenzao. Aidha kuonyesha kutambua huduma wa waimbaji hao kanisa lao pamoja na viongozi waliwaandalia waimbaji wa kwaya hiyo mlo maalumu siku ya jumapili iliyoisha kuonyesha kutambua mchango wao mkubwa katika kumuinua Kristo kupitia huduma yao katika kanisa hilo la The Brooklyn Tabernacle.

Mchungaji kiongozi Jim Cymbala akizungumza na wanakwaya

Mwalimu Carol Cymbala akinena na wanakwaya wake

Kundi la wapigaji vyombo vya muziki wa kwaya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wao Carol Cymbala

Baadhi ya waimbaji waliojikuta wamevalia nyeusi wakaamua kupiga picha pamoja
Vivyo hivyo kwa waliojikuta na nyeupe wakapiga picha pamoja
Mchungaji Jim na Carol Cymbala na baadhi ya waimbaji
Baadhi ya waimbaji wa sauti ya tatu wa kwaya hiyo

Baadhi ya waimbaji wa kwaya hiyo ambao pia wanaimba kwenye kikundi cha watu wachache katika kwaya hiyo wakiongozwa na Brandon Camphor katikati©BTCTazama moja ya kazi ya zamani bora kabisa toka kwao BTC "Nothing Impossible"


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.