SO LOST WITHOUT YOU KUTOKA KWA WORSHIP HOUSE 7 NDIO CHAGUO LA GK LEO

Baadhi ya waimbaji wa Worship House mapema jana asubuhi wakijiandaa kwa recording yao©WH
Katika chaguo la GK kwa siku ya leo tupo jimboni Limpopo Afrika ya kusini ndani ya kanisa la Christ Worship chini ya Bishop Dagada. Tumekuchagulia wimbo kutoka kundi "So lost without You" kutoka toleo la 7 la kundi la Worship House washindi wa tuzo ya kundi bora la muziki wa injili Afrika ya kusini kupitia tuzo za Metro FM zilizofanyika mapema mwaka huu.

Worship House limejinyakulia tuzo mbalimbali kwa uimbaji wake wa kupiga miziki mingi kwa kitamaduni sambamba na uvaaji wao. Wimbo huu ni kiitikio kutoka wimbo maarufu wa "Air I breath" ambao kundi hili umeimba kwa mtindo wa regge. Ambapo kwasasa kuanzia jana na leo wanarekodi toleo lao la 13 kanisani kwao Shiyandima Limpopo Afrika ya kusini. Tunakutakia jumapili njema


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.