SOMO: KUZIMU WANATOKA JEHANAMU HAWATOKI - MCHUNGAJI KILIMA

Mchungaji Kiongozi Ufufuo na Uzima Tanga John Kilima
SOMO: KUZIMU WANATOKA JEHANAMU HAWATOKI

Kuzimu imetajwa mara nyingi sana kwenye biblia hivyo tuna kila sababu ya kujifunza kwa habari ya kuzimu. Lakini neno jehanamu limeandikwa mara 12 kuonyesha kwamba haina kazi nasi kwa sasa kwani imeandaliwa kwaajili ya shetani na malaika zake.
Kuzimu ni makao makuu ya utawala wa shetani ufunuo 12:7-12
Shetani alipotupwa kuzimu akaanza kuishambulia dunia na kuvuna watu wengi waingie kuzimu. Kuzimu ni shaimo (shilo), shimo lipo hapahapa duniani.
Kuna mashimo madogomadogo ambayo yapo chini ya mawakala wa shetani. Mashimo hayo yaweza mapango, dari, uvungu, nk na yanapata nguvu kutokea kuzimu (shimo kuu). Mashimo hayo yanaweza kuachilia nguvu yenye kushika maisha ya watu, ndoa, kazi, biashara, elimu n.k.
Kuzimu pia inaitwa moyo wa nchi. Yona2:3
Yona alishushwa hadi moyo wan chi na samaki kwa muda wa siku tatu, Yesu pia alikwenda hata moyo wan chi akamnyang’anya shetani funguo za kuzimu na mauti..
Ufunuo9:2
Shimo hili (kuzimu) linaweza kuachilia mambo fulaanifulaninkutokea kwenye ufalme wa giza. Shimo likaachilia wadudu wawadhuru watu wote wasiokuwa na alama.
Ukiona mikosi, balaa, kukataliwa, magonjwa n.k ni mambo yanayotokea kwenye shimo hilo.
Kuzimu ni roho, roho inaweza kugeuka na kuwa na kuwa shimo. Kuzimu ina mikona, moyo, mdomo, na pia ina malango yenye makomeo yake.. makomeo hayo yanaweza kufungia ndoa ya mtu, biashara, kazi, au jambo lolote.
Zab18:15
Kuzimu ina kamba, inafunga mabo ya wanadamu. Kuzimu inaweza kugeuka na kuwa makao.
Zab49;14
Kama hizo hushikilia watu wasitoke kwenye vifungo walivyofungiwa.
Kuzimu pia ina mdomo zaburi141:7,
mithali 7:27…… njia ya kuzimu
kuzimu in tama na kiu isaya 5:14
watu wanakufanya mapatano na kuzimu isaya 28:15
upo mkono wa Mungu wa kurudisha vyote. Yesu alipokufa akaenda kuzimu akafanya kazi ya uinjilisti makaburi yakafunguka kaonekana miili ya watu waliokufa na wengi wakamwendea Yesu.
Leo hii watumishi wa Mungu ndio mkono wa Mungu wa kuwatoa watu walioko kuzimu. Mkono huo unaweza kurudisha kila kitu kilichoibiwa na shetani ndoa, elimu, biashara, kazi, nyota safari n.k
Isaya 42:22
Shetani huwa anatabia ya kuangalia kutokea kuzimu. hata sisi tuliookolewa kuna baadhi ya vitu vyetu amevifungia kuzimu hivyo tuna kila sababu ya kuishambulia kuzimu ili kurudisha vyote. Baada ya kutokea Siklagi na wake wa Daudi kutekwa pamoja na watu wengine na mali zinyine na mji kuchomwa moto, daudi akamuuliza je akifuata jeshi atalipata? Mungu akamjibu utapata na bila shaka utapata vyote hivyo Daudi akaliendea jeshi na kuwapata wake zake na kila kilichotokwa alikirudisha. 1samuel30:8
Hata sisi tunaweza kusimama kama Daudi tukaishambulia kuzimu na kurudisha mali, elimu, afya, biashara, nyota, ndoa, kazi, ustawi na chochote kile navyo vikarudi. Tumepewa mamlaka hivyo tunaweza, usiogope simama upigane hakika utapata vyote.
Uhalisia wa kuzimu
Luka16:13
Mtu anapokufa, roho huwa ina kila kitu macho, mdomo, mikono na viungo vingine kama ilivyo mwilini.
Lazaro akaonekana kwenye kifua cha Ibrahimu (paradise) na tajiri akaonekana katika shimo akiteseka (kuzimu)
Luka 23:43.
Unapokufa tu unatua mahali unapostahili. Yesu akamwambia Yule mhalifu aliyetubu ‘ leo hii utakuwa pamoja nami peponi’. Hivyo hata mtu anapokufa akiwa dhambini anatua kuzimu moja kwa moja sawasawa na alivyoishi duniani.
Watu wanaweza kwenda kuzimu na kurudi. Ndivyo watu wengi wanavyofanya leo hii wale walioingia mapatano na kuzimu. Fahari na mambo mengi vyaweza kuwekwa kuzimu.
Isaya14:11
Unaweza kuwa na fahari lakini ikashushwa kuzimu.
Watu na vyote vilivyoko kuzimu vinaweza kurudi kutoka kuzimu. Unaweza kuwa unafanya mambo Fulani (biashara) lakini inakwenda kwa ugumu kumbe imefungiwa kuzimu au ndoa haendi vizuri kumbe imefumgiwa kuzimu, leo vitarudi vyote kwa Jina la Yesu.
Zaburi86:13, 16:3
Matendo 2:27
Isaya42:22
Jehanamu
Jehanamu imeandikwa mara chache.
Mathayo5:21, 5:29-30
Kuna vitu vinavyosababisha mtu kwenda jehanamu. Shetani anatumia njia yoyote ili aende na mtu jehanamu. Jehanamu ni kwaajili ya shetani na malaika zake.
Kuzimu ni kituo cha biashara, kuna watu wameibiwa vipawa vyao na kuviweka kuzimu na kuwauzia watu waendao kuzimu.
Ufunuo18:11
MAOMBI
Kwa mamlaka ya Jina la Yesu leo nafuata vitu vyangu vyote vilivyoko kuzimu, naishambulia kuzimu yote mapango yote, nayaendea mashimo yaliyomeza ndoa yangu, kazi, elimu, tumbo la uzazi, watoto, biashara……..(endelea kutaja). Imeandikwa umemeza mali nyingi lakini Bwana atakutapisha vitoke tumboni mwako, nakutapisha vyote kwa Jina la Yesu. Kama Daudi naviendea vyote vilivyotekwa kutoka kwenye maisha yangu nna hakika nitavipata.

AMEN
INFORMATION AND MEDIA MINISTRY
UFUFUO NA UZIMA- TANGA

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.