SOMO : UNDANI WA MAOMBI (1) - MCHUNGAJI MADUMLA

Mchungaji Gasper Madumla


Ilikuwa ni majira ya mchana ambapo bwana Hamisi mwenye nyumba alipokuwa nyumbani kwake.Baada muda fulani kupita mpangaji wake mmoja alirudi kutoka matembezini,maana alikuwa na wapangaji wanne. Gafla,yule mpangaji akaenda kuchota maji kama ilivyo desturi yake. Bomba la maji lilikuwa uwani,wapangaji wote pamoja na familia ya bwana Hamisi walishirikiana matumizi ya bomba,na choo pia.

Pale ambapo mpangaji alipokuwa akienda kuchota maji,bwana Hamisi alikuwa akimchungulia dirishani mwake kuona jinsi atakavyonaswa na mtego wake aliouweka pale bombani. bwana Hamisi kumbe! alikuwa ni mchawi mkubwa sana,mwenye kujificha ficha katika uchawi wake. Alimuwekea uchawi mpangaji wake akanyage kisha achanganyikiwe.

Basi,mpangaji alipoenda kuchota maji,gafla akakanyaga yale mauchawi,akakinga maji,kisha akaenda zake bafuni kuoga,akatoka bafuni yupo salama na akaendelea na kazi zake.Sasa,bwanaHamisi alipoona mpangaji hajadhulika hali amekanyaga zile dawa,alafu wala hakuchanganyikiwa alishangaa! Akajiuliza na kukosa jibu,maana hajawai kumtega mtu asitegeke,akapigwa na butwaa!

Akaendelea kumsikilizia kuona labda dawa itafanya kazi baadae,lakini wapi! Yule mpangaji wake alipomaliza shughuli zake akatoka akiwa mzima na kurudi akiwa mzima wa afya.

Kitu kimoja alichokosa kikijua huyu bhana Hamisi mchawi ni kwamba maisha ya mpangaji wake yalikuwa katika maombi. Maombi yalichukua nafasi kubwa kiasi kwamba hakudhulika; pale penye mtego wa uchawi, Ndiposa nikaliangalia neno la Mungu lisemavyo;

“ watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; “ Marko 16:18

Hivyo,uchawi wa mwenye nyumba ulidunda na wala haukufanikiwa kwa sababu,huyu ndugu alikuwa ameokoka na ni mwombaji mzuri. Baada ya kuyasikia hayo,nikajifunza kwamba iko haja ya kujifunza juu ya undani wa maombi.

Undani wa maombi ni somo pana,lenye kufafanua mambo ya ndani ya kuhusu maombi. Undani wa waombi

Fundisho la maombi ni kati ya mafundisho ya msingi sana ya mkristo. Kila mkristo anapaswa kuwa muombaji,na mlinzi wa kiroho mahali alipo;Hivyo basi ili ufanyike mwombaji au mwombezi huna budi kujifunza kiundani kuhusu somo hili la maombi. Neno “mwombezi” linamaana ya mtu anayesimama siku zote kuombea wengine na kutengeneza palipo bomoka.

Maombi ni somo lisiloepukika kwa mkristo. Fikiri maisha yanakuaje pasipo maombi? Kilicho bora katika maisha ya mwanadamu ni maombi,ni afadhali mtu akunyime vyote lakini asikunyime muda wa maombi. Maombi ndio kila kitu!

Kumbuka ya kwamba;kiu uliyonayo ya kukua kiroho,kiu ya ushindi wa kiroho,kiu ya kumiliki mambo yako mbali mbali,yote hayo yamefichwa katika maombi. Hivyo,utagundua kwamba maombi yamebeba siri za mambo mengi sana.

Madhumuni makubwa ya somo hili la maombi ni kukupa maarifa kamili kuhusu maombi kwa ujumla na kukufundisha namna ya kuomba vizuri. Ili sasa,ubadili ufahamu wako kuhusu maombi. Sasa twaweza kuanza kwa kujikumbusha kile kilichoandikwa katika Yakobo 4:1-3

“ Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.“

Kupitia andiko hili,tunajifunza kwamba yapo makundi mawili ya watu;

01.Watu wasioomba,

02.Watu wenyekuomba vibaya.

Lakini pia lipo kundi la watu,wenye kuomba vizuri. Kundi hili ni kundi zuri sana. Sasa,ili tuweze kulifikia kundi hili;ni lazima tujifunze yafuatayo:

01.Nini maana ya maombi?

02.Kwa nini tunaomba.?

03.Aina za maombi.

04.Jinsi ya kuomba vizuri.

05. Mifano ya waombaji waliofanikiwa.

06.Mazingira yafaayo katika maombi

07.Mazingira yasiyofaa katika maombi.

08.Mkao mzuri wa maombi/Mikao katika maombi.

09.Sababu ya kutojibiwa maombi yako.

10.Faida za maombi.

11.Mathara ya kuishi bila maombi.01.MAOMBI NI NINI?

Nilipojaribu kuangalia tafsiri kamili ya maombi,nikagundua maana tatu za neno hili maombi. Nazo ni kama ifuatavyo;

(i) Maombi ni mazungumzo kati ya Mungu aliye hai na watu wake tukimshukuru,tukimuabudu,tukitubia dhambi zetu,na kuomba mahitaji yetu binasfi na ya wengine;

Tafsiri hii ya maombi inaeleza hasa nini maana ya maombi,na inatupa picha kwamba maombi sio“omba omba” yaani maombi sio kila siku uhitaji kutendewa kwamba “Baba nipe,Baba nipe…” Bali maombi yana husika pia na kushukuru,kuabudu,kusifu,kutubia kisha ndipo kuomba haja zako binafsi. Neno hili “maombi” limetokana na neno la kiingereza “praise” yaani “kusifu,kumuinulia BWANA sifa”ITAENDELEA..

Kwa mawasiliano ya maombi na ushauri,piga +255 655 11 11 49.

Mch.Gasper Madumla.

Beroya Bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.