WANAKWAYA NA WAPIGAJI KATIKA VIKUNDI VYA KWAYA JISALIMISHENI, UJUMBE WENU HUU

Malagasy Choir kutoka Madagascar ©TV sur Erdre

Ujumbe unaoenda kuusoma ni maombi ambayo yameandaliwa na mwalimu, mtayarishaji muziki na mshauri wa masuala ya uimbaji ndugu John Mtangoo.. Maombi haya yametokana na masuala mbalimbali waliyotaka wanakwaya kutoka sehemu mbalimbali Tanzania waliotaka kuombewa kwaya zao kuhusiana na nyanja mbalimbali walizozitaja kupitia ukurasa wa Facebook ya mwalimu huyo ambaye aliandaa kutokana na maombi hayo pia na uzoefu wake katika vikundi vya uimbaji.. Nina hakika kama tabia tajwa unazo pia ukiungana naye katika maombi haya utasaidia kwa kiasi kikubwa kuponya kikundi chako na wewe binafsi. Karibu

KUOMBEA ENEO LA FIKRA KWA WAIMBAJI
Waimbaji wengi wanaona sifa kuwa wajinga.
Ujinga ni nini?
1. Unatumia muda wako kumuimbia Mungu usiyempenda wewe ni timamu?
2. Majungu, uongo, umbeya, fitina na chuki ni marafiki wa kwaya. Mojawapo ya utamu wa kwaya ni masengenyo. Huu ni utimamu?
3. Unaamua kutoka nyumbani unaenda kuimba kwa kujitolea, unachelewa mazoezi, ukifika ni kusababisha magomvi na chokochoko huo ni upuuzi bwana kwani lazima uimbe?
4. Kwaya inaimba wewe ambaye hujui kuimba unataka kujitapa kwa masifa na kiburi huu ni zaidi ya ujinga!
5. Wewe unaimba kwaya ukahaba ndio tabia yako na sehemu kubwa ya kwaya wamekufunua utupu wewe ni timamu kweli?
6. Wewe unayetegemea fedha kidogo ya kwaya iliyopatikana kwa jasho jingi unaiba, unadokoa, unarudisha kwaya nyuma acha upuuzi bwana!
7. Unajifanya mwanamuziki maringo mengi unajifanya unajua, unaringia kundi, unataka ubembelezwe acha ujinga WANAOJUA SIKU ZOTE HAWAJUI! ASIYEJUA HUWA HAPOTEI NJIA!
Unajua kuna wapuuzi wanaenda kwaya na viroba mifukoni!
JIANGALIE SANA MWENENDO WAKO. MUNGU ANA MAWE YA KUYATUMIA. Usijifanye mjuaji kwenye kazi ya Mungu.
NA KATIKA MAMBO YOTE TWAJUA YA KWAMBA MUNGU HUFANYA KAZI NA WALE WAMPENDAO

KUOMBEA WANAMUZIKI
YAKOBO 1:7 - Kila kipaji chema hutoka kwa Mungu. 
Mpiga bass mkongwe Abraham Laboriel
Kwaya nyingi kwa miaka mingi zina changamoto eneo hili. Mimi pia ni mnufaika mkuu wa changamoto hii. Nakumbukwa kwaya yangu ya kwanza kuisaidia nilikuwa kidato cha kwanza na nililipwa 2500/=. Ada yangu ili kuwa 5000 hivyo ningeweza kujisomesha.
Kuwadhibiti wanamuziki wakati uhitaji wao ni mkubwa kwenye jamii ni kazi kubwa sana.
JARIBU KUTUMIA NJIA HII ILI KUWADHIBITI WANAMUZIKI
1. Wahimize ama wawezeshe kusoma ama kupata ujuzi wa ziada nje ya Mziki.
2. Wawezeshe kupata ajira za kudumu hivyo kuondoa utegemezi wao kwenye Mziki.
3. Kama ni lazima waishi kwa Mziki wafungulie mradi unaofanania na taaluma yao mfano Studio au Darasa la kufundisha Mziki.
4. Wape nafasi ya kujitambua kuwa wao ni sehemu ya kundi na sio watu maalum nje ya kundi.
Kuna kwaya nyingi tu eti wanamuziki hawatoi michango wengine hadi sare wanashonewa. Hiyo sio sawa.
NAMNA BORA YA KUPATA WANAMUZIKI WAPYA.
1. Tumia watoto wadogo walioko kwenye eneo husika ama kanisa husika. UMRI wa kuanzia miaka 12 ni sahihi sana.
2. Kwa idadi ya watu wazima walioko jaribu kufundisha wengi kadri uwezavyo utaambulia wawili watatu wa kukusaidia. Hii ni kwa kusaidia kwa muda mfupi.
3. Jaribu kujenga uhusiano na wanafunzi hasa wa shule za secondary zilizoko karibu na wewe. Hata kama wanaweza kuwa hawatulii lakini kuna siku watakufaa.
Kumbuka kundi la Mungu ni kudumu hivyo usipende kutafuta mafanikio ya muda mfupi.
KUTAFUTA MWALIMU WA KUKUSAIDIA.
Tafuta MWALIMU mwenye nia ya dhati ya kuendeleza vipaji. Walimu wengi wakuajiriwa hawapendi hii dhana. Lakini kwa asili kuna walimu wengi tu wanaopenda kuinua vipaji. 
Barikiwa sana.

Mwigizaji maarufu Whoopi Goldberg katika sinema ya Sarafina akiimbisha choir 


KUOMBEA WALIMU WA KWAYA
Msitari wa kutafakari
JEREMIAH 1:5 - Kabla sijakuumba nalikujua, kabla hujatoka kwenye tumbo la mama yako nalikutakasa(ordained).
UHUSIANO WA MATENDO MABAYA YA WALIMU NA UBORA WAO
Unataka kujua kama MWALIMU wa kwaya uliye naye ni sahihi na atasaidia katika utunzi bora wa nyimbo? Hizi ni tabia za walimu bora.
1. Mlevi, mzinzi ana kiburi ama yote kwa pamoja. Kuna MWALIMU mmoja nampenda sana. Anatunga nyimbo bora sana ila ni mnywa gongo mzuri sana.
2. Hana wivu wa maendeleo ama maisha take hayana mipango anaishi kwa ajili ya siku iliyoko mikononi mwake .
3. Ana ushawishi kwa kundi na hii hupelekea wanawake kujirahisisha kwake.
Kuna walimu wengi sana wanapenda kuishi kwa fadhila za kwaya hivyo wanazuia mafanikio yao na uzee huwakuta hawajajiandaa. Msingi wa mawazo huwafanya kuwa walevi kypindukia.
Kwa ujumla kuna uhusiano mkubwa sana wa tabia za walimu na tabia za Samsoni wa kwenye Biblia.
Ualimu ni wito wa kuzaliwa tokea tumboni na Ibilisi hulijua sana hili. Walimu wengi wanajua sana neno la Mungu. Jiulize ufundi wa kuunganisha Ujumbe unatokaga wapi? Ni KIPAWA cha Roho Mtakatifu kabisa. Na shetani anajua nikimgusa MWALIMU nimeua kundi. Machozi ya wadada kwa walimu ni sehemu ya mkakati wa kuzimu.
Siri kubwa ya walimu wa kwaya wakimjua Mungu na kusoma Biblia na MAOMBI huishia kuwa Wachungaji. Hivyo utaona umuhimu wa kuwaombea walimu. Wamebeba kusudi zito sana la utumishi. Tabia zao ovu ni msingi wa uharibifu wa kuzimu.
Barikiwa sana.

KUOMBEA WAIMBAJI WOTE.
KUTAMBUA THAMANI YA WITO WAKO.

Kama kuna kitu kinakera walimu wengi ni wanakwaya wengi kutokujali mazoezi. Unaandaa mipango Fulani ya kiuimbaji lakini kundi moja linakuja Leo lingine kesho. Hakuna ujinga unaokera kama kwaya kujaa kwa sababu ya safari ama kurekodi hasa video. Mimi naamini Baraka za waimbaji hazionekani sababu hii. Mungu hajatuita kuwa waburudishaji. ISAYA 61. Habari njema itatoka wapi kama hatutilii mkazo mazoezi. Vipofu wataona nini kama kila siku tunakwazana kwa kudharau wito tulioitiwa. Wafungwa gani wakuwekwa huru kama sisi wenyewe hatujawekwa huru tunatumikia sifa na maonesho ya kibinadamu.
Naongea na waimbaji wavivu, wategevu na wasiojitambua. Hujalazimishwa kuja kuimba. Kama hutaki kaa nyumbani.
Mungu anataka kutumia vipawa alivyotupa kwa faida huku tukiukomboa wakati.
Mungu akupe kujua thamani ya wito wako.
Barikiwa.

Moja ya usafiri wa kwaya ya Uinjilisti Forest KKKT Mbeya

KUOMBEA UCHUMI WA KWAYA- FEDHA YA KUREKODI
MASOKO YA MAUZO YA CD/DVD
JE NI KWELI KUNA FAIDA YA KUSAMBAZIWA CD/DVD?

Mwaka 2006 nilirekodi video. Nikangia mkataba Wa kukopeshwa recording na fedha taslim kwa minajili ya kazi kujilipa. Kilichotokea kila baada ya mezi 6 nilikuwa nikiletewa mrabaha(royalty) Wa 5600 au 7000. Baadaye nikaambiwa nitafute namna ingine ya kulipa deni. Nduti One Stop mkenya huyu yeye aliiona DVD yangu akaniita na kunipa cash 2500,000/=. Msambazaji mmoja alikuwa ananipa fedha hata kitimoto haitoshi mwingine akanipa fedha nyingi lakini isiyorudisha gharama.
Wengi wamekuwa wananiuliza Juu ya masoko ya kazi zao. Nataka nikuhakikishie kumpa msambazaji kazi ni hasara isipokuwa kwa wateule wachache.
Chukulia hivi: msambazaji atakuba shs 500 kwa DVD hivyo unahitaji angalau DVD 10,000 angalau gharama irudi. Hiyo ni hadithi kwa Tanzania. Najua wako wasanii wachache na kwaya chache mno wanazidi hapo.
Pili wasambazaji wengi sio waaminifu. Najua wapo ambao Mimi sijakutana nao.
Tatu haki miliki hakuna hivyo uchomaji Wa DVD mtaani unaua soko.
NJIA RAHISI YA KUONGEZA MAPATO YA CD/DVD
1. SIKU YA UZINDUZI
2. TEMBELEA MAKANISA MENGI UWEZAVYO ILI UUZE MWENYEWE.
Chukulia hivi: wastani Wa kutengeneza DVD in 2000 ukiuza kwa 5000 faida ni 3000. Jitahidi kuuza angalau 3000 PCs utaona faida.
Ukishafika idadi ya cd / DVD 3000 ndio ukomo Wa kusambaza binafsi, gharama zimerudi na faida Juu. Kisha sasa tafuta msambazaji.
Mwisho kujulikana kwa kikundi kunahitaji uvumilivu na maombi sana. AMANI, umoja na shkamano msingi Wa mafanikio. Msisahau kuandaa na matamasha yatakayozidi kutangaxa kundi.

Kwaya ya Uinjilisti Sayuni KKKT Kinondoni Dar es salaam
KUOMBEA RECORDING ZOTE
Kuna sababu tatu za kurekodi.
1. Kutunza kumbukumbu
2. Kusambaza habari
3. Kuongeza kipato
Unapoamua kurekodi lazima uzingatie hayo mambo. Shida ya vikundi vingi tunapambana kwenye sababu ya tatu ya kuongeza kipato huku tukisahau kwamba mambo hayo matatu yanategemeana. Tunaposema kutunza kumbukumbu tunamaanisha ni urithi wa nyimbo unaowekwa kwa faida ya vizazi vijavyo. NATAKA KUSISITIZA KWAMBA DUNIANI HAMNA WIMBO MBAYA WALA MZURI BALI KUNA WIMBO NINAOUPENDA NA NISIOUPENDA.
Tukisema kueneza habari maana yake ule Ujumbe uenee. Iwe kusikilizwa radioni, ama kutazamwa kwenye TV ama CD vyovyote vile Ujumbe unaenea. Hivyo kuwa makini na kuandika Ujumbe wenye mashiko.
Tukisema kuongeza kipato hapo ni biashara. Ujanja wa kujua Ujumbe gani unasubiriwa ama kutegemewa na jamii ndiyo faida yako. Kuongeza vionjo bora vya kimziki kunaongeza faida ya soko. Kuna vikundi vinawekeza kwenye kucheza sana nataka kuwaambia MTAFURAHISHA JUKWAA LAKINI HAKUTAKUWA NA FAIDA BALI KUJICHOSHA TU.
NAMNA BORA YA KUCHAGUA STUDIO
1. Chaguo studio ambayo umeshasikia kazi zake na wewe mwenyewe ukazipenda.
2. Waulize wale waliokwisha Fanya kazi wakupe uzuri na ubaya wa hiyo studio.
3. Usitembee tembee kuuliza uliza studio na bei zake utapotea tu.
4. Walimu wengi wa sasa wanalazimishia studio wanazotaka si kwa sababu ya ubora Bali kwa sababu ya masilahi wanayopewa na studio.
5. Studio kama studio si bora ila yule FUNDI aliyekurekodi na kuchanganya ndiye bora. Ukijua Fulani ndiye bora mfuate hata kama atakurekodi chini ya muembe.
6. Tofautisha ubora wa muimbaji binafsi na kwaya. Usiende studio iliyompa umaarufu muimbaji binafsi kama wewe ni kwaya tafuta mahali kwaya bora ilipotoka.
Nilishawahi kusuluhisha kwaya moja ya VIJANA iliyotaka kwenda kurekodi kwa P-FUNK kwa sababu nyimbo nyingi za bongo fleva zilikuwa zinafanya vizuri sana. 

MWISHO KAZI BORA HAITOKANI NA STUDIO BALI INATOKANA NA MAANDALIZI BORA. USIKIMBILIE STUDIO KAMA HUNA ZOEZI LA KUTOSHA.

Mwalimu na mshauri wa mambo ya uimbaji John MtangooShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.