YNA WA THE PROMISE AWEKA PEMBENI UIGIZAJI AJIKITA KUMCHA MUNGU NA KULEA FAMILIA YAKE

Kristine Hermosa Sotto na familia yake
Ili kuonyesha kwamba anafuraha tele na maisha yake ya ndoa, mwigizaji nyota wa Ufilipino ambaye ameokoka, Kristine Hermosa almaarufu kama YNA katika tamthilia ya The Promise, ameamua kujikita zaidi na familia yake baada ya kutangaza anatarajia kupata mtoto wa tatu katika ndoa yake na mwigizaji mwenzake Oyo Boy Sotto.

Mwigizaji huyo aliamua kutangaza ujauzito wake mpya hivi karibuni, wakati ambao mashabiki wake
Jericho na mkewe Kim
walitegemea kumuona akirudi tena kwenye uigizaji baada ya mtoto wake wa pili aitwaye Kaleb Sotto kuanza kutembea. Aidha mashabiki hao walikuwa na imani ya kumuona mwanadada huyo amabye yeye na mumewe ni wafuasi wazuri wa wokovu, baada ya mpenzi wake wa zamani ambaye kwasasa ni mume wa mtu Jericho Rosales almaarufu kama Angelo kuwa tayari kuigiza tena na Kristine na kwamba wanatarajia jambo hilo kutokea karibuni.

Hata hivyo msimamo wa binti huyo kuweka familia yake mbele dhidi ya fani yake umepokelewa na kupongezwa na wengi licha ya kuumia kumkosa kwenye uigizaji, wakidai kwamba ni msichana wa kuigwa nchini humo kutokana na tabia nzuri aliyonayo, na kuachana na umaarufu na kuweka mbele familia yake. Kristine na mumewe Oyo wamejaaliwa watoto wawili mpaka sasa kwenye ndoa yao pamoja na mtoto mwingine wa kiume waliyemchukua kutoka kituo cha watoto yatima ili kumlea, na kufanya kuwa na idadi ya watoto watatu mpaka sasa huku mtoto mwingine yupo mbioni.

Familia ya bwana na bibi Oyo Boy Sotto, maalumu kwa kijana wao alipotimiza mwaka mmoja


Unaweza kusoma na kutazama harusi ya Angelo kwa kubonyeza Hapa

Harusi ya Yna Bonyeza HapaShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.