BABA AMCHOMA MWANAYE MPAKA KIFO KWA KUBADILI DINI

Kijana akiwa katika hali ya maombi (si kijana aliyechomwa) ©Christianteens

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Abubakar Malagara (36) raia wa nchini Uganda na muumini wa dini ya kiislamu amemuua mwanaye wa miaka 9 kwa kumchoma hadi kufa baada ya mtoto huyo kubadili dini na kuwa Mkristo na kukaidi kufunga katika kipindi hiki ambacho waumini wa dini hiyo wanafunga kuadhimisha ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Morning Stars na kuripotiwa pia na Christian Post umeripoti kwamba mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Nassif Malagara alikutwa na baba yake akila chakula kwa jirani siku ya tarehe 9 June baada ya siku mbili za mfungo bila kula chochote tangu abadili dini. Awali inadaiwa mtoto huyo alimkabidhi Kristo maisha yake siku nne kabla ya tukio hilo June 5 baada ya kuchukuliwa na jirani yake kuhudhuria kanisani nje ya kijiji chao.

Kwa mujibu wa mchungaji ambaye hakutajwa jina lake kwasababu za kiusalama, amesema mtoto huyo alitulia mpaka mwisho wa ibada na kumfuata mchungaji huyo na kumwambia kwamba anataka kumpokea Kristo awe mwokozi wa maisha yake kitendo ambacho mchungaji huyo amedai kusita kidogo lakini alipoona mtoto huyo amemaanisha alichosema alimuombea na mtoto huyo kuondoka.

Aidha mchungaji huyo amedai kwajinsi wanavyoelewa kuna uwezekano mtoto huyo aliwaeleza ukweli baba yake na mama yake wa kambo aitwaye Madina Namwaje kwamba hataki kuhudhuria madrasa (darasa la vijana wa kiislamu) au kujihusisha na mambo ya dini yake hiyo ya zamani. Akaongeza kwamba baba yake na mama yake wa kambo walipatwa na hasira kwa kugundua mtoto huyo amebadili dini na kuwa Kristo.

Licha Malagara kubadili dini wazazi wake walijua kwamba atafunga ramadhani lakini mtoto huyo aliweza kufunga siku mbili tu lakini akashindwa na kuamua kwenda kwa jirani kula chakula na kukamatwa na baba yake na kuanza kuchapwa, lakini alifanikiwa kumkimbia baba yake na kwenda kujificha kichakani lakini baba yake aliweza kumkamata. Mtoto huyo aliongeza kwamba alichukuliwa na baba yake mpaka nyumbani ambako alimfunga kwenye mti wa ndizi na kuingia ndani ya nyumba kisha kutoka na mti. Amesema mti aliokuwa amefungiwa ulikuwa tayari umenyauka na kushika moto ambao ulisababisha madhara makubwa mwilini mwake.

Na kwamba ni majirani ndio waliosikia mtoto huyo akipiga kelele na kwenda kumfungua kutoka katika mti huo na kumpeleka hospitali kwa matibabu ambako alieleza kisa hicho kwa shida. Ambapo baba yake alikamatwa na polisi baada ya wakazi kutoa ripoti ya tukio hilo. Ambapo Malagara aliungua sehemu mbalimbali za mwili wake kwa mujibu wa mmoja wa matabibu wa hospitalini hapo aliyefahamika kwa jina la Walwawo Zubari. Tabibu huyo alidai mtoto huyo alianza kupata nafuu taratibu lakini alihitajika kuhamishiwa hospitali nyingine kwa wataalamu zaidi.

Majirani wamedai baba yake aliachiwa ka dhamana na kwamba mmoja wa ndugu zake na mtoto huyo alikubali kumchukua mtoto huyo akiruhusiwa kutoka hospitalini kwa matibabu. Pia inadaiwa mtoto huyo akaanza kupata jumbe za vitisho kutoka kwa mtu asiyejulikana ingawa kwa mujibu wa jirani aliyempeleka mtoto huyo hospitali anadai jumbe hizo zitakuwa zimetoka kwa baba mzazi wa mtoto huyo kupitia simu ya muumini mwingine wa dini ya zamani ya mtoto huyo. Ujumbe huo ulidai utavuna ulichopanda na itakuwa fundisho kwa wengine, Uislamu ni kinyume na ulichokifanya.

Matukio ya aina hiyo yameendelea kutokea nchini Uganda mara kwa mara licha ya kwamba asilimia 85 ya wakazi wa nchini humo ni Wakristo... Visa vingine GK itakupatia hivi karibuni.

Tazama "Not Forgotten" ya kwao Watoto Children Choir kutokana kanisa la Watoto UgandaShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.