CHAGUO LA GK BADO KITAMBO KIDOGO KUTOKA KWA KWAYA KONGWE NA BORA NCHINI
Kupitia chaguo la GK jumapili ya leo ni katika kukutia moyo wewe msomaji wetu ambaye unapitia magumu na mapito mbalimbali katika dunia hii. Kumbuka bado kitambo kidogo mambo yote yatakuwa sawa tena cha muhimu ni kuzidisha mwendo ukimtumainia Kristo ambaye ndiye tegemeo letu na muweza wa yote. Wimbo unaitwa "Bado Kitambo Kidogo" kutoka kwa kwaya kongwe nchini ya Kurasini SDA Choir ambao wanapatikana nyuma ya viwanja vya maonyesho vya Mwalimu JK Nyerere zamani Sabasaba jijini Dar es salaam. Barikiwa utazamapo wimbo huu

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.