CHAGUO LA GK NI WIMBO UNAOPENDWA NA KUREKODIWA NA WAIMBAJI WENGI AFRIKA YA KUSINI


Leo tupo nchini Afrika ya kusini katika kukuletea chaguo la GK, kuna waimbaji wengi nchini humo ila leo tumekuchagulia mwanakaka Sechaba Pali ambaye katika wimbo huu wa kitabuni licha ya kuwahi kuuimba na kurekodi katika kanda yake binafsi lakini hapa alikaribishwa na kushirikishwa kwenye DVD ya kusherehekea miaka 30 ya huduma ya malkia wa muziki wa injili Afrika mwanamama Rebecca Malope. Katika rekodi yake alitiwa nguvu na waimbaji wa Joyous akiwemo marehemu Lihle Mbanjwa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka juzi

Wimbo unaitwa Lona Baratang wimbo huu wakutia moyo na kuwataka watu kuishi chini ya mwamba
hodari ambaye ni Kristo umerekodiwa na waimbaji wengi wakiwemo Joyous Celebration, Pastor Benjamin Dube katika album yake mpya, Sechaba, Rebecca na wengine wengi. Kama hufahamu, Sechaba ni zao la Joyous Celebration enzi hizo na nikati ya waimbaji ambao kundi hilo linajivunia kwakuwa tangu amalize mkataba nao amekuwa akifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini humo. Tunakutakia jumapili njema
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.