FURAHA NDANI YA JOYOUS CELEBRATION BAADA YA NYOTA WAO KUFUNGA NDOA

Hlengiwe Ntombela akiwa tayari kwa harusi
Jumamosi ya jana ilikuwa ya furaha kwa familia ya kundi maarufu la muziki wa injili barani Afrika, Joyous Celebration mara baada ya kiongozi wake wa muziki wa kundi hilo mwanakaka Siyanqoba Mthethwa kufunga ndoa na mmoja wa waimbaji hodari kundini humo mwanadada Hlengiwe Mtombela katika harusi ya kufana iliyohudhuriwa na waimbaji mbalimbali wa kundi hilo.

Siya pamoja na Hlengiwe wamekuwepo kwenye mahusiano kwa muda mrefu kabla ya kuhitimisha uhusiano huo kwa kufunga ndoa hapo jana na kupata hongera nyingi kutoka kwa waimbaji wenzao ambao hawakuweza kuzuia furaha hiyo kwa kuweka picha mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii hususani Facebook.
Maharusi wakiwa wamekumbatiana


Bheka, Sylvester na Sibu wakiwa na bwana harusi
Hlengiwe Ntombela na Sylvester Funani

Tazama wimbo wa kwanza uliompa jina bibi harusi Hlengiwe Ntombela


Wakati huohuo mwimbaji nyota aliyewahi kuvuma na kundi hilo mwanadada Ntokozo Mbambo wa Mbatha naye hapo jana alifanikiwa kunyakua tuzo ya mwimbaji bora wa muziki wa injili nchini humo kupitia album yake mpya ya Spirit and Life ziitwazo South African Music Awards (SAMA) zilizofanyika siku ya jana ambapo kama ilivyokawaida mwanadada huyo alipata pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki na waimbaji wenzake hususani waliofanya kazi pamoja kwenye kundi la Joyous Celebration. Lakini pia kundi hilo lilipata tuzo kupitia DVD yake ya 19 kwa kuongoza kwa mauzo nchini humo

Ntokozo akiwa na Sylvester mara baada ya kupokea tuzo yake
Ntokozo Mbambo akiwa mwenye furaha na tuzo yake


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.