GOODLUCK SANDY KUWEKA WAKFU DVD YAKE MWEZI JULAI

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Arusha Goodluck Sandy anatarajia kuiweka wakfu albam yake ya tatu ya nyimbo za kusifu na kuabudu, iliyo katika mfumo wa sauti za picha (video).

Katika mahojiano ha GK, Goodluck ameeleza kuwa albam yake imebeba nyimbo kumi na mbili ambazo zimejaa upako wa aina yake utakaokutanisha watu na mahitaji yao kwa Mungu.

Albam hiyo iko katika mfumo wa DVD, kazi ikiwa imeongozwa na John Maulid wa JM Media.

Endelea kutufatilia Gospel Kitaa kwa habari zaidi kuhusiana na uzinduzi huo.


Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.