HARUSI YA DADA YETU MTANZANIA NA SHEMEJI MGHANA ILIVYOTIA FORA UINGEREZA


Sio siku yake kwa tukio kama hili kwa upande wa GK kuweka taarifa za harusi bali imetubidi kukufahamisha kuhusiana na video fupi ya harusi iliyotokea kutazamwa sana na watu kupelekeana kupitia mtandao wa Facebook na Vimeo... Ni kwamba harusi hii ni yadada yetu mtanzania aliyeolewa na shemeji yetu kutoka Ghana ambao kwa pamoja ni wakazi wa jijini London nchini Uingereza.

Bwana harusi anaitwa Gabriel Deku na dada yetu anaitwa Annabella. Harusi hii ilifanyika mwezi uliopita katika kanisa la St Martin in the fields jijini London na kuhudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wa maharusi.. Kilichofanya video hii kutazamwa zaidi ni chozi ama kilio kilichoangushwa na bwana shemeji alipomuona dada yetu anaingia kanisani tayari kwa ajili ya ndoa.

Wapenzi hawa ambao kwasasa ni mke na mume wameelezea historia ya mapenzi yao yalivyoanza kupitia video mbalimbali zinazopatikana katika channel yao ya YouTube ambako ndiko video hii tulipoichukua. Lakini pia kilichotusukuma zaidi kuweka harusi yao ni kutokana na namna walivyomshirikisha Mungu katika safari yao ya uchumba mpaka ndoa. Chini tumekuwekea baadhi ya picha na video yenyewe.......Hongereni sana maharusi
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.