MABINTI 19 WAUWAWA KIKATILI KWA KUWAKATALIA MAGAIDI NGONO


Mji uliokuwa na takriban watu milioni mbili na nusu kwamujibu wa sensa ya mwaka 2014, ni mji ambao unashuhudia mauaji ya kila namna kila iitwapo leo, na hivi karibuni, mauaji ya mabinti 19 wa Jamii ya Yazidi ambao ni Wakristo, waliuwawa kwa kuchomwa moto mbele ya umma, wakiwa wamefungiwa ndani ya banda la nondo; kosa lao - kukataa kushiriki ngono kama mateka wa kundi la kigaidi la Islamic State, ISIS.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa mji huo wa taifa la Iraq, mbinu kama hiyo imekuwa ikitumiwa na magaidi wa kikundi hicho, ili waweze kwatia hofu mateka wengine kusudi wakubaliane na masharti yao bila hiyana.

Mabinti Jamii ya Yezidi katika kambi ya wakimbizi ya wakimsubiri mwambata wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na wakimbizi, Angelina Jolie kwenye kambi ya wakimbizi iliyopo Midyat, Uturuki. ©Reuters/Umit Bektas
Umoja wa Mataifa umeshaweka bayana kwamba mauaji ya jamii ndogo kama ya Yazidi ni ya halaiki, na Marekani pamoja na mataifa kadhaa ya Magharibi yameingilia kati kwa kutuma vikosi vyake dhidi ya kikundi hicho cha ISIS.

Licha ya tukio hilo la mauaji kufanyika hadharani, hakuna mtu yeytote aliyethubutu kutoa msaada, kwa kuhofia kuunganishwa na kundi hilo la mabinti 19.

Katika hatua nyingine imeripotwa kwamba magaidi hao wamekuwa wanawauza mabinti hao kupitia kurasa za mitandao ya kijamii wakiuzwa kwa dola 8,000 sawa na takriban milioni 16 kwa yeyote anayehitaji mtumwa wa ngono.

Jamii ya Yazidi ama kwa jina lingine Yezidi, inafikia idadi ya watu 800,000 pekee, na jina lao likiwa na maana ya 'Uzao wa Mungu'. Kwa mujibu wa historia yao, wamekuwa wakipata mateso licha ya kuwepo kwao toka enzi na enzi.

Unapoombea matukio ya dunia, haya ni baadhi ya mambo unayoweza kupeleka mbele za Mungu.

Vyanzo: Yezidi Truth | Christian Post |

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.