MAKALA: KUTANA NA WORSHIP IN ADVANCE (WIA) KUTOKA DODOMA


Sehemu ya waimbaji wa Worship in Advance, Dodoma.
Worship in Advance Connection (WIA Connection) ni kikundi kilichoanza kama kikundi cha sifa na kuabudu kilichojumuisha wanafunzi wa vyuo vikuu waliookoka na wenye mzigo wa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji pamoja na vijana wengine ambao sio wanafunzi lakini wenye mzigo huo pia bila kujali madhehebu yao.

Kundi hili limeanzishwa mnamo tarehe 27/05/2015 kama “Joint Praise Team” kwa ajili ya ibada ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na Oliva Molel na Moses Lesilwa ambao kwa pamoja walikua wnafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma. Baada ya kufanya huduma hiyo Mungu aliwapa mafunuo ya kukifanya kikundi hicho kuendelea na akatupatia jina hili la Worship In Advance lenye maana ya “kumuabudu Mungu katika viwango vikubwa na vya juu”. 

Baada ya kuanzisha kikundi hiki, walipata upinzani kutoka katika baadhi ya vikundi vya dini na hiyo ilipelekea baadhi ya wanachama wao kuacha kundi ili kutumikia majukumu mengine waliyokabidhiwa na vikundi vyao vya dini. Lakini wanamshukuru Mungu kwa sababu aliwatutia nguvu na kuwatusaidia kuendelea mbele mpaka hapa walipofika. Kwa sasa kundi la WIA linawashiriki 25 ikiwemo wapigaji, waimbaji, designers  na washauri.         

Baada ya kuhudumu kwa muda, Mungu aliwapa maono ya kuanzisha WIA Connection ambayo kwa kupitia hiyo wameweza kufanya mambo mengi zaidi mbali na ibada za sifa na kuabudu na hivyo kulifanya kundi la Worship In Advance kufanya kazi chini ya WIA Connection. Baadhi ya maono ya WIA Connection ni kama;

1.      Kufanya ibada na matamasha ya kusifu na kuabudu.
Hili ni kusudi kubwa kabisa la kundi hili lenye azma ya  Kuwafikia watu hususani vijana na kuwaongoza kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli na kuwafanya kuiona Nguvu na Uweza wa Mungu unaopatikana katika kumsifu na Kumwabudu Mungu kunakofanyika kwa viwango vya juu na ustadi mkubwa”. 


Lakini pia kupitia makongamano ya kusifu na kuabudu tumedhamiria kuihubiri Injili ya Yesu iletayo wokovu.

Mbali na kusudi hilo, pia tunategemea kufanya mambo yafuatayo ili kuujenga ufalme wa Mungu na kugusa maisha ya watu kwa ujumla:
  • Kuandaa makongamano ya Neno la Mungu.
  • Kuandaa warsha mbalimbali zinazohusiana na maisha ya vijana. (hili litafanyika kwa Motivational/Inspirational Talkings ambazo zitawainua vijana katika maisha yao ya kiroho na kimwili pia.)
  • Kufanya matamasha kwa nia ya kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu
  • Kufanya matamasha kwa nia ya kuwasaidia watumishi wa Mungu wanaofanya kazi katika mazingira magumu nk.

Mpaka sasa Worship In Advance wamefanikiwa kufanya ibada mbili kubwa za kumsifu na kumwabudu Mungu zilizojumuisha wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma na vyuo vingine vya hapa mjini Dodoma wanaotokea katika vikundi mbalimbali vya dini vilivyoko katika vyuo hivyo. Lakini pia Mungu ametusaidia kua chanzo cha umoja katika vikundi hivyo vya kidini vilivyoko katika vyuo vyetu katika kushiriki ibada kwa pamoja.


Utumishi ndani ya WIA ni kwa njia ya kujitoa na si kwa ajili ya mapato. Mara zote wanapoamua kufanya matukio yetu hua tunatumia pesa zetu wenyewe kama wanafunzi kwa sababu mpaka sasa hatuna mfadhili yeyote anayewasaidia lakini Mungu mwenyewe ndiye awawezeshaye. Lakini pia ili kuandaa ibada hizi imewagharimu muda wao mwingi wa kufanya mazoezi ili waweweze kufanya kwa ustadi mkubwa ili kutimiza adhima yetu. Ikumbukwe kua WIA sio kikundi cha kidini kwa hiyo hata vyombo vya kufanyia mazoezi hutegemewa kutoka katika vikundi vingine vya dini kitu ambacho kwa wakati mwingine imekua ngumu kuvipata kwa wakati unaohitajika na wakati mwingine hii imepelekea kutembea mwendo wa zaidi ya kilomita 3 wakati wa usiku ili tu kufanya mazoezi. Lakini yote katika yote wanamshukuru Mungu maana kwao ni faraja kubwa kutumika. 


Mambo makubwa yaliyowasaidia WIA kufika hapa walipo ni kwa kumuamini Mungu katika mambo yao lakini pili ni maombi kuhusiana na kile wakifanyacho. Mara zote wamekua wakimuomba Mungu kabla ya kufanya tamasha lolote na hata wakati wa maandalizi pia ili kuwasaidie katika yote wanayopitia. Lakini pia jambo kubwa linalowafikisha hapa walipo ni Umoja, Ushirikiano na Kujitoa (self comitment). Mambo haya ndio nguzo kuu ya kundi lao, na kuafanya kuendelea mbele kila iitwapo leo.

WIA wametegemea kufanya mengi makubwa katika siku zijazo. Maombi yako ni ya muhimu kwao. Na Mungu akubariki.

Unaweza kuwasiliana na kuwapata WIA kupitia anuani zifuatazo:
Facebook: worshipinadvance
Instagram: worship_in_advance

Zifuatazo ni picha kutoka katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa WIA yaliyofanyika katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma usiku wa ijumaa  tarehe 10 mwezi wa sita mwaka 2016 kama ambavyo GK ilikuwepo na kukuletea tukio zima hili, ungana nas.
 


Keki iliyoazimisha Mwaaka mmoja wa WIAWIA Katika Kusifu

Muda wa sebene ukipamba motoKatika uwepo
Kwa picha Zaidi Bofya Hapa 


Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.