MWANAMKE LIBYA ALIVYOLIPA GHARAMA KWA KUMFUATA KRISTO MAISHANI MWAKE

Wanawake wa Kikristo dhehebu la Coptic  Libya wakiomboleza kuuwawa kwa waume zao ©Charismanews

Jina lake anaitwa Maizah alikuwa hana jinsi zaidi ya kukimbia nchini kwake Libya kwenda mafichoni. Alipigwa sana na kundi la wanaume wenye ndevu na kupewa ofa ya kuolewa kuwa mke wa nne kati ya mmoja wa wanaume hao ili wasimpige.. Akajua kwamba kwakuwa amebadili dini na kuwa Mkristo akikataa kuolewa basi hata familia yake itamuua, hivyo kukimbia ilikuwa njia pekee kwake.

Kwasasa binti huyu yupo kwenye umri wa miaka ya 20, binti huyu bado anateseka na kitendo cha kupigwa na wanaume hao pamoja kwamba amepata makazi huko nchi za magharibi lakini bado anaogopa kwamba kuna mtu atajua anapoishi sasa na kwenda kumchukua. Ingawa muonekano wake kwasasa umebadirika kidogo ukilinganisha na zamani, anavaa msalaba ambao ni kitu muhimu kwake. Akiwa amekaa kwenye sofa za rangi nyekundu ndani ya chumba kidogo , akazungumza maisha yake yalivyokuwa akiwa kwao nchini Libya.

"Mungu yupo wapi?
Nilipokuwa na miaka 8 nilimuuliza mama yangu, Mungu yupo wapi, anafananaje? sio vizuri kuuliza haya maswali mama yake alimjibu kwa ukali, inabidi uombe msamaha, kwasababu Mungu hana umbo.. Lakini Maizah hakuwa ameridhika na jibu la mama yake.


Niliwaona mabinti wakienda msikiti uitwao Sufi kusoma na kushika Quran, Nilitaka kwenda nao, familia yangu haikupinga, lakini baadaye msikiti ulifungwa. Nikiwa na miaka 9 nilikwenda katika msikiti wa Salafist. Imamu aliponiona nimevaa suruali alianza kunipiga, nilikimbia, nilikuwa namtafuta Mungu, lakini huyu Imam alinishangaza. Kutokana na kitendo hicho sikwenda msikitini tena alisema Maizah


Alipokuwa binti, alianza tena kuutafuta ukweli kuhusu Mungu, Mtu mmoja aliniambia kuna msikiti mwingine, watu wa huko ni watofauti, nilikwenda huko nikiwa nimejifunga hijab kichwa kizima, hata mikono yangu ilikuwa imezibwa. Mara ya pili, niliingia nimevaa suruali, nilitaka kujua nini kitatokea, walinikubali nilivyo, nilijifunza sana Quran niliupenda msikiti huo. Lakini anasema furaha yake ilikuwa yakitambo, ni pale tu walipoanza kumwambia ana umbo zuri, kwanini asijifunike zaidi?, walitaka niuzibe mwili wangu zaidi.

Msikitini alivaa kiislamu, lakini alipotoka matembezi na rafiki zake alikuwa huru kuvaa anavyotaka, pale msikitini wakagundua tabia yake na kumwambia alikuwa anamdanganya Mungu, ukweli hicho sicho nilichokuwa nakitaka, lakini nilianza kufahamu kwamba hata wao walikuwa wanamdanganya Mungu. "Niliwaona wakifanya vitu vibaya, niliwahi kumsikia mmoja wa viongozi akidanganya kwenye simu na kugundua kwamba alikuwa muongo, alinihuzunisha kitendo kilichomfanya Maizah kuhama msikiti na kuamua kuachana na kuishi maisha ya dini tena.

'Njia Kweli na Uzima'

Mwaka mmoja baadaye mwanzoni mwa mwaka 2011 Maizah alikutana na nguvu ya kiroho ambayo hakuweza kuisimulia ilivyokuwa. Siku moja akiwa analia kitandani kwake, alihisi mtu mmoja anamshika miguu yake. Chumba kilikuwa giza lakini ghafla niliona mwanaume aliyekuwa anang'aa kama mwanga, hakuwa anaonekana kama mtu, alihisi kwamba hakuweza kumgusa mtu huyo, alisimama pembeni yangu, nilihisi furaha ndani ya moyo wangu kwasababu ya uwepo wake ' Mimi ni njia, kweli na Uzima' alisema mtu huyo, kisha akawa ameondoka.

Wakati hili limetokea ilikuwa ni wiki mbili kabla mapigano ya wenyewe kwa wenyewe hayajaanza Libya, mabomu yalipoanza jirani na nyumbani kwao aliamua kukimbilia nchini Misri na familia yake.

'Nuru ya Libya'

Akiwa Misri alijuana na Mkristo ambaye alikuwa jirani yao, mwanamke huyo alimwalika, lakini familia ya Maizah wakamuonya binti yao kujihusisha na mwanamke huyo kwasababu ya imani yake. Kukatazwa huko kulimfanya Maizah atake kujua zaidi, mwanamke huyo alikuwa mkweli kwake, alimtaka aambiwe kuhusu Yesu, maneno aliyoambiwa yaliugusa moyo wa Maizah moja kwa moja, alimuamini mwanamke huyo, akaomba aonyeshwe Biblia, ilikuwa mara yake ya kwanza na kwamba aliiogopa. Maizah alianza kumtembelea mwanamke huyo kila siku, siku moja alimwambia kuhusu mwanaume aliyemtokea alipokuwa Libya, mwanamke huyo alimjibu kwamba huyo alikuwa Yesu, na kumuonyesha wapi palipoandikwa maneno aliyoambiwa na Yesu.

Baada ya muda, Maizah akahisi kwamba ilikuwa wakati muafaka kwake kuieleza familia yake kuhusu imani yake mpya kwa Yesu, jirani huyo alimbariki na kumwambia yeye Maizah atakuwa nuru itakayowaangazia watu wa Libya. Safari yake ya pili nchini Misri alibatizwa kwakusaidiwa na rafiki yake Mmisri ambaye aliweza kumuunganisha na familia ya Kikristo nchini Libya. Maizah anasema hata kabla ya utawala wa Kiislamu nchini kwake, ilikuwa kuhudhuria kanisani Libya ilikuwa haiwezekani kwa Walibya. Kanisa lililoruhusiwa lilikuwa kwa raia wa kigeni tu, kwahiyo wakawa wanakutana kwa siri kwa miaka miwili.

Mwaka 2013 familia aliyokuwa akisali nayo walikamatwa, mchungaji aliyemuunganisha na familia hiyo alimuunganisha na familia nyingine ya Kikristo. Maizah alionywa kwamba polisi walikuwa wanamtafuta yeye walipokamatwa rafiki zake, kwakuwa waliona karatasi yenye jina lake na kumfanya akimbilie nchini Misri kwa mara nyingine. Familia yake walifanya kila waliwezalo kumpata na kujikuta akiishia nchini Uturuki, akiwa na mipango ya kukimbilia Ulaya.

'Nyumba ya Usalama'
Siku moja anasema alimpigia simu mama yake lakini ikajibiwa na dada yake aliyemjibu kwamba mama yao hali yake sio nzuri kwani alikuwa amepooza, aliamua kurudi nyumbani kwasababu alitaka awe pamoja na mama yake. Anasema alipokuwa uwanja wa ndege alikuta familia yake ikiwa inamgonjea kama vile hakuna chochote kilichotokea, anasema alipoingia nyumbani alishangaa kumuona mama yake akiwa amesimama na kujua kwamba alikuwa amedanganywa. Kaka yake akamwambia kuna watu waliotaka kuzungumza naye sebuleni na kwamba hakutakiwa kuogopa kwakuwa atakuwa pamoja naye. Sebule ilijaa wanaume wenye ndevu na kuvalia kanzu ambao walianza kumuuliza maswali

Anasema mmoja wao alianza kwakumpiga kibao usoni, huku akidhania kaka yake atamlinda, walimkamata na kuanza kumpiga sana lakini anasema akahisi kwamba alikuwa analindwa kwakuwa akuhisi maumivu kabisa. Waliendelea kumpiga, ambapo mmoja wao aliamua kuzungumza, Maizah jina lako lipo kwenye listi ya watu wanaotakiwa kuuwawa, nitakupa ofa, naweza kukuoa, nina wake watatu na wewe utakuwa mke wa nne, ukikubali tutaachana na haya yote alisema mwanaume huyo.

Anasema alishutushwa na ofa hiyo aliyopewa lakini alimua kukubali ili kupata muda, aliomba kukutana na daktari kabla ya kuolewa, mwanaume huyo alikubali ila hakutaka aende hospitali ya walibya badala yake alipelekwa Tunisia huku wakimwekea ulinzi, na kusema kwamba hakukua na namna ya kutoroka. Lakini amesema alikuwa naikumbuka namba ya simu ya mchungaji kwa kichwa, akisaidiwa na daktari aliweza kutoroka na kupata nyumba ya kujihifadhi. Familia yake ikaanza kumtafuta lakini nyumba aliyoko ikawa imemuhakikishia usalama haswa kwani hawajaweza kumpata.

Maizah sio jina lake hailisi, aliweza kuondoka na kukimbilia nchini za Magharibi ambako hata hivyo anasema anaogopa kuna watu wanamtafuta.
Habari hii imetafsiriwa kutoka World Watch Monitor

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.