PATA CHAGUO LA GK LENYE VIWANGO KUTOKA KWAYA YENYE VIWANGO

Baadhi ya wababa kwaya ya MKC wakiwajibika wakati wakirekodi video mpya ©MKC
Chaguo la GK jumapili ya leo tupo maeneo ya Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es salaam ndani ya kanisa la Pentekoste ambako tunakutana na moja kati ya kwaya bora kabisa katika medani ya kumtangaza Kristo kwa njia ya uimbaji.

Hawa si waengine bali ni Mwananyamala Kisiwani Choir (MKC) ambao kutoka kwao tumekuchagulia wimbo uitwao "Moyo Wangu" ni moja kati ya nyimbo bora kabisa zilizowahi kutolewa na kwaya hii iliyojaa waimbaji wenye vipaji vya juu katika uimbaji.

Ambapo baadhi ya waimbaji wake wamewahi kuwa na band iliyowahi kutamba miaka ya 2000 ya Amana Vijana Center (AVC Band). Tunakutakia baraka za Mungu utazamapo na kusikiliza ujumbe kutoka kwa waimbaji hawa. Barikiwa

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.