SOMO: DUNIA IMEHARIBIKA, NA KILA MWENYE MWILI AMEJIHARIBIA NJIA YAKE


Mambo mengi yanayofanyika ndani ya maisha ya mwanadamu siyo sawa na vile Mungu anavyotaka ambapo kila moja ameishika njia yake potofu na inawezekana msomaji wa ujumbe huu na wewe njia yako imeharibika kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu; hebu mrudie Mungu ili uwe salama. Mwanzo 6:12-13

1. Kwa sababu ya kuharibika dunia hofu ya Mungu haipo tena mioyoni mwa watu watu wanaishi dhambini  na  wako mbali na Mungu na inawezekana ndugu yangu ukawa ni miongoni mwa watu wa namna hii. Ni hatari sana kwako kukosa haofu ya Mungu kwa sababu kunaweza kukupelekea kufanya lolote ambalo lipo kinyume na Mungu. Na Mungu kachungulia toka mbinguni aone kama kuna mwenye akili anayemwabudu yeye na kaona wengi wako mbali. Zaburi 14:2-3

2. Pia watu wamemkataa Mungu ndani ya mioyo yao na huku  wanaonekana kuabudu wakati mioyo yao iko mbali na Mungu. Maana wamekataa kutawaliwa na Mungu mioyoni mwao. Hii inaonekana kupitia maisha wanayoishi au kwa njia zao na matendo yao yanamkana Mungu na inawezekana ni miongoni mwa watu wa namna hii; hebu ondoka kwenye hali hii kubali kumwabudu Mungu kutoka ndani ya moyo wako  Mathayo 15:7-9

3. Wengine mioyo yao  imeharibika mana wekataa magizo ya Mungu   ya kutoa zaka ndani ya maisha yao na huku wanasema wanataka kwenda mbinguni   nahii ni tatizo la watu wangi ndani ya kanisa na kwenda kinyume na magizo ya Mungu ni dhambi hivyo kwa kukataa kwako kutoa fungu la kumi hautaenda mbinguni kama ulikuwa hautoi anza sasa ili uwe salama Kumb 14:22 Malaki 3:8-10

4. Dunia imeharibika, mana watu wanalikataa neno la Mungu hawamtaki Mungu wa kweli mioyoni mwao maana kulikataa neno ni kumkataa Mungu na hauwezi kuwa salama pale unapolikataa neno la Mungu maana Mungu husema nawe kupitia neno. Zaburi 107:20

5. Baada ya dunia  kuharibika Mungu akaona aitengeneze Safina ili mwanadamu aingie na awe salama. Kuna watu walikuwa wanamcheka Nuhu wakati anajenga Safina, wakaona kama amechanganyikiwa; na ndiyo ilivyo sasa watu wanaona kama kuokoka ni kuchanganyikiwa na wengine wanawacheka walokole inawezekana ukawa ni miongoni mwa watu wanamna hii utakuwa upo kwenye hatari sana katika maisha yako maana yale yaliyowapata wale waliomcheka Nuhu wakati anajenga Safina yaweza kukupata.

6. Waliomcheka Nuhu wakati wa kuitengeneza Safina wakapata shida ya kufutiliwa mbali wakati wa gharika. Baada ya mvua kubwa kunyesha wakatamani kuingia kwenye Safina wasiweze. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa watu wengi wanaokataa kuokoka sasa maana watateseka maisha yao milele watatamani kuokoka neema itakuwa haipo.

7. Mioyo imeharibika watu hawataki suluhu na wengine hawataki kusamehe  na huku wanataka kwenda mbinguni na biblia inasema usipo samehe nawe hautasamehewa  hivyo huwezi kwenda mbinguni kama haujasamehewa dhambi zako. Hivyo ni vizuri ukawasamehe wengine ili nawewe usamehewe Mungu. Marko 11:25-26

8. Ni watu wachache tu ndio walioingia kwenye Safina na wengine waliangamia, ndivyo itakavyokuwa siku ya unyakuo. Ni wachache watakaonyakuliwa  na wengi wataangamia kwenye ziwa la moto

9. Wenye haki ndio walioingia kwenye safina na hata mbinguni watakao ingia ni wenye haki pekee yao mana yake waliookoka tu bila kujali anaabudu wapi maadamu Yesu amekuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yao na wanaishi kulingana na maagizo ya Mungu  Mwanzo 7:1-7

10. Safina ya leo ni Yesu Kristo, mwanadamu utakapoingia ndani ya Yesu utakuwa salama kama Nuhu alivyokuwa salama baada ya kuingia kwenye Safina. Inawezekana haujaokoka, Safina ya sasa ni Yesu kristo na wewe utakapoingia utakuwa salama kama ilivyokuwa kwa Nuhu.
Mungu alifanya agano na Nuhu la kuingia kwenye safina na hata sasa mtu anapookokoka anafanya agano na Mungu la kuingia mbinguni na hili ni lamuhimu kwako kama bado. Mwanzo 6:18
Fanya kama Mungu anavyokuambia; hiyo ndiyo salama yako maana Nuhu alifanya kama alivyoambiwa na Mungu akawa salama

11. Ili uende mbinguni ni lazima uzaliwe mara ya pili na si vinginevyo Yohana 3:3-5

12. Unapomwamini Yesu unakuwa umepita mauti na kuingia kwenye uzima wa milele. Yohana 5:24 ,6 :40 ,48-51
 
13.  Na kwa sababu ya kuharibika kwa njia za watu, wengi wanakufa dhambini maana dhambi ni mauti na usipo mwamini Yesu hauna uzima ndani yako na utakufa katika dhambi zako   Yohana 23-24

Namshukuru Mungu kwa kunipa ujumbe huu na pia wewe msomaji naamini Mungu kasema nawe jambo

Tunakukaribisha kuteka Baraka ya kuhubiri Injili pamoja na mimi kupitia Redio ya Dodoma FM 98.4 kila Jumamosi saa moja hadi saa mbili usiku. Na pia ninahubiri mitaani ambapo maono ni kuwafikia wasiofikiwa 

Mchungaji Oscar  Mwanyanje
S.L. P. 2036, Dodoma
0752473707 /0713 312797
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.