SOMO: ULICHOKIOTA KITAONEKANA - ASKOFU GWAJIMA

Askofu Dkt Josephat Gwajima wa Ufufuo na Uzima
Neno ndoto limeandikwa mara 86 ndani ya Biblia. Lakini Jumla ya ndoto zilizootwa ndani ya biblia ni ndoto 23 na watu walioota ndoto hizo ni watu 15 tu ndani ya Biblia. Miongoni mwao walioota baadhi yao kwenye Biblia wameota ndoto zaidi ya mara moja, ndio maana ndoto ziko nyingi kuliko waota ndoto wenyewe. Wachungaji wengi duniani hawasemi habari ya ndoto kwa sababu ya andiko hili:

Mhubiri 5: 3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno, 7 Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu.”

Husema hawawezi kuhubiri kuhusu ndoto kwa sababu mtu huota ndoto kwa sababu ya shughuli nyingi za kila siku na maneno mengi ambayo mtu hunena. Kwa kawaida ndoto za shughuli nyingi hutokea pale tu kama mtu ni fundi wa barabara anaota ndoto za shughuli ya barabarani, au mwalimu anaota unafundisha darasani, au kama mtu ni daktari anaota anatibu mgonjwa n.k
hizo ndizo aina ya ndoto za kila shughuli za kila siku.
Lakini kama wewe ni mwalimu lakini umeota upo baharini unatupa unatupa mayai unazama hiyo siyo ndoto ya shughuli za kila siku, kama wewe ni Rais au Waziri au Mbunge na unaota unakimbizwa na mbwa hiyo sio ndoto ya shughuli za kila siku, kama wewe ni mfanya biashara unaota ndoto umetumbukia shimoni hiyo sio ndoto ya kila siku.

Imeandikwa;
Hesabu 12: 6 “Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.”

Mungu anasema na watu katika ndoto. Huwezi kuyadharau yaliyosemwa na Mungu mwenyewe ukamtukuza Solomoni aliyeandika kitabu cha mhubiri ,kwasababu Mungu ni mkubwa kuliko Solomoni na amesema akitokea mtu kati yenu nitasema naye kwa njia ya ndoto.

1Samweli 28: 6 “Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii, 15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.”

Samweli anasema Mungu hamjibu tena wala kwa ndoto wala kwa manabii, hapa ina maana Mungu alikuwa anamjibu maombi yake kupitia hapo kabla lakini hakuweza kumsikia ndotoni.
Ebimaleki aliota ndoto ikatokea, Yakobo aliota ndoto ikatokea, Labani aliota ndoto ikatokea, Yusufu ‘waziri mkuu’ aliota ndoto mara mbili ikatokea, Mnyweshaji wa mfalme wa Misri aliota ndoto ikatokea, Mwokaji wa Mfalme aliota ndoto ikatokea, Mfalme Farao aliota ndoto ikatokea, Askari wa jeshi la midiani aliota ndoto ikatokea, Sulemani mwana wa Daudi aliota ndoto ikatokea, Ayubu mtu wa Mungu aliota ndoto ikatokea, Nebukadreza Mfalme wa babeli aliota ndoto mbili zikatokea, Danieli aliota ndoto ikatokea, Yusufu mumewe mariamu aliota ndoto nne zikatokea, mamajusi walionywa katika ndoto ikatokea, mke wa pilato aliota ndoto ikatokea. Tumeona wafalme wawili wameota ndoto zikatokea kumbe na viongozi wakubwa nao wanaweza kuota ndoto na zikatokea.

Unaweza kuota ndoto ya ajabu ikakusumbua sana ukiwa ndotoni na unapoamka ukasema kumbe ni ndoto tu halafu ukadharau na kuendelea na maisha, wewe si wa kwanza kusema hivyo Farao naye alisema.

Mwanzo 41: 5 “Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.”

Unaweza ukawa umeota upo juu ya daraja na mtu amekusukuma ukaanguka ile unakaribia chini unaamka, unaota nyoka anakukimbiza anakufuata ile anakukaribia akung’ate unaamka, inawezekana umeshawahi kuota ndoto una gari, umejenga, umepata hela nyingi na ukaamka. Watu wengi siku hizi huota ndoto za ajabu na huwa wanaziona kama ndoto tu za kawaida.
1:wafalme 3: 5 “Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.”

Sulemani naye aliota Mungu amemwambia; omba chochote nikupe ,ndipo akaamka na kusema kumbe ni ndoto tu, Sulemani alikua mfalme mwenye hekima kuliko wote, alipata ndotoni, alikuwa tajiri kuliko watu wote, alipata ndotoni. Sulemani aliishi sawasawa na ile ndoto aliyoiota na kilitokea.

Wewe ulichokiota kama ni kizuri au kibaya kitakuwa vilevile. Kama ni kibaya kifanyie kazi ili kisitokee kwa jina la Yesu.

Mwanzo 20: 3 “Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.”

Abimeleki alimwoa mtu kumbe alikuwa mke wa mtu na Mungu alimtokea kwenye ndoto ili amwache la sivyo atauwawa.

BAADHI YA WATU WALIOWAHI KUOTA NDOTO KATIKA BIBLIA
1.YAKOBO ALIOTA NDOTO TATU.

Mwanzo 28: 12 “Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.”

Mwanzo 31: 10 “Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka.”

Mwanzo 31: 11 “Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.”

2. YUSUFU NAYE ALIOTA NDOTO AMBAYO NI MAARUFU SANA
-Ndoto aliyoota Mnyeshwaji wa Mfalme

Mwanzo 40: 12 “Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu.”

3. MFALME FARAO ALIOTA NDOTO MARA MBILI.

Ni ileile lakini iko kwenye mfumo tofauti.

Mwanzo 41: 5 “Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema.”

Mungu alimthibitishia kwamba neno lile aliloliota litakuwa vilevile. Leo hii watu wengi wanaota ndoto lakini wanadharau na wanakuja kulalamika baadaye wakipata matatizo sababu wameshindwa kufahamu sauti ya Mungu alivyoongea naye. Ndoto ni moja ya njia ya kusikia sauti ya Mungu.

Waamuzi 7: 13 “Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini.”

Askari wa midiani waliota ndoto. Waliota Gideoni amekwenda kuwashambulia kambi yao wakati Gideoni yupo kichakani aliwaskia askari hao wakisimuliana kwamba ameota ameona mkate umeshuka kutoka mbinguni umeanguka kwenye kambi yao na kuwashambulia wote na Gideoni aliposikia akiwa kichakani alikwenda kuwapiga wote usiku uleule. Unaweza kuota ndoto ikatokea siku hiyohiyo kama ndoto hii ya askari hawa wa mideani. Pia unaweza kuota ndoto ikachukua muda mrefu kutokea kama ilivyotokea kwa Ayubu.

Ayubu 7: 14 “Ndipo unitishapo kwa ndoto, Na kunitia hofu kwa maono”.

4. DANIEL NAYE ALIOTA NDOTO IKATOKEA
Danieli 7: 1 “Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.”

Watu wengi siku hizi wanaota ndoto za ajabu tofauti nna ndoto za kwenye biblia. Huwezi kuota kwenye Biblia mtu anakimbizwa na tembo mpaka, maisha yamebadilika mpaka na ndoto zimebadilika, unakuta mtu anaota anafunga harusi yupo ndani ya maji, unaota unasoma shule lakini umeshamaliza shule, unaota unakula nyama.
Ndoto zilitabiriwa kwenye biblia.

Yoeli 2: 28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono”

Jina yoeli maana yake ni Mungu ashikaye maagano na watu wake. Yoeli aliishi miaka mia tatu kabla ya Kristo. Alitabiri kwamba kwenye nyakati za mwisho watu wataota ndoto na wengine kuona maono.

Baada ya Yesu kuzaliwa Petro aliyarudia yale maneno aliyotabiri Yoeli.

Matendo ya mitume 2: 17 “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.”

Haya maneno yalisemwa karne ya kwanza ,akisema hizi ni nyakati za mwisho, kama wakati ule ulikuwa ni wakati wa mwisho je nyakati hizi si za mwisho zaidi!!.

Unaweza ukaota umefanya biashara ukafanikiwa na baadaye wakaja wezi wakakuibia ukafilisika.

Unaweza ukawa umeota ndoto ukaisahau wewe sio wa kwanza hata Mfalme Farao aliota akasahau. Sababu zipo mbili

I. Asili ya ndoto zinaweza kuruka zisipatikane tena ndiyo asili ya ndoto. Unaota kitu kizuri na unakisahau.

Ayubu 20: 8 “Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku”

II. Shetani ana kawaida ya kuiba ndoto. Maelekezo ya ndotoni ni ya muhimu sana yanaweza kuelekeza maisha yako. Ndoto zote huwa zinaishia na kuamka lakini kuna ndoto zingine unaota usingizi unakata unaamka. Unapoota ndoto ukiamka kitu cha kwanza iandike.

Habakuki 2:2 “Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.“
Unapoota ndoto usihangaike kumsimulia mtu hiyo ndoto sababu inaweza kutokea asubuhi. Unapoamka kutoka ndotoni usitafute tafsiri ya ndoto bali jiulize ni jambo zuri umeliota au ni jambo baya, ni ya pesa au ni ya umaskini, ni ya baraka au ni ya huzuni, usipoteze muda kumtafuta mtu akuambie maana yake, maana yake ni Mungu ameongea na wewe.

Kuna ndoto ambazo unaziota mara nyingi, yani zinajirudia . Mwingine ameota ameaibika na ameshindwa kutoka. Mwingine ameota amebanwa sehemu na ameshindwa kutoka ,ndoto kama hizo unatakiwa uangalie mwenyewe kama ni mbaya au ni nzuri.
Kuna mnyweshaji na mwokaji waliokuwa wanafanya kazi kwa mfalme farao ambapo wote waliota ndoto zikatokea na mmoja aliota akaambiwa atanyongwa mpaka afe lakini akakaa kimya hajui cha kufanya mpaka akaja akafa kwa kunyongwa. Watu wengi siku hizi wanaota ndoto mbaya wanakaa kimya na mpaka ndoto zao zinakuja kutokea.

NDOTO NGUMU ILIYOOTWA KWENYE BIBLIA
Alitokea mtoto mmoja aliitwa Yusufu alikua mtoto wa mwisho kwenye familia yake. Alikuwa ni myahudi lakini aliota amekuwa waziri mkuu wa misri kitu ambacho kilikuwa ni jambo kigumu.
Aliota ndoto ambayo ilikuwa ngumu sana kutokea mpaka alipoiadisia kwa ndugu zake wakamwingiza shimoni, (ukiingia shimoni ingia pamoja na ndoto yako) ndoto kubwa zinahusishwa na kusalitiwa na kuuzwa, ukisalitiwa na kuuzwa wewe linda ndoto yako. Ndoto kubwa zinaenda pamoja na kusingiziwa , lakini wewe baki na ndoto yako. Ndoto aliyoota Yusufu ilichelewa mpaka akaingia gerezani lakini baada ya kutoka gerezani alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye hatima ya ndoto yake. Ndoto kubwa zinaenda pamoja na kuingizwa gerezani lakini wewe ishikilie ndoto yako mpaka utakapotoka na itatimia kwa jina la Yesu.

Yale yote uliyokosea Mungu amekusamehe kwa jina la Yesu na ndoto zako zinatimia.

MAANA YA KUOTA MARA MBILI AU ZAIDI
Ayubu 33: 14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”

Mungu anasema anasema na wewe katika ndoto kwakuwa hujali na yeye anakupenda sana anaileta ndoto ile ile kwa namna tofauti.

Mungu huwa anafundisha kwamba jambo hilo ni lazima litokee. Mungu anaweza kuleta mambo kwa namna ambayo hukuwaza wala hukutegemea.

Mungu alishawahi kumwambia nabii atembee uchi na atembee kuwaambia watu kuwa wako uchi mbele za Bwana kama yeye alivyo uchi, pia Mungu alishawahi kumwambia mtu asitokee kwenye mlango bali achimbe chini atoke nje.

Mfalme Daudi aliwahi kutembea na mtu nje ya ndoa, jambo hilo lilimchukiza Mungu mpaka akamwadhibu Daudi lakini aliyekuja kuzaliwa ni Sulemani ambaye yeye ndiye aliyekuja kuwa mfalme japo kuna watoto wengine wa ndani ya ndoa walikuwepo lakini Mungu hakuwachagua.

Mungu aliwaambia wana wa Israeli waifuate nguzo ya moto ambayo iliwapeleka mpaka baharini japo kulikuwa na njia nyingine ya kupita lakini Mungu alikuwa ana mpango wa kuwaangamiza wamisri na wakaangamia.

Ndani ya mzoga huwa kuna inzi na minyoo lakini kwa Mungu mzoga hutoa asali ndani yake. Ileile hali uliyokuwa nayo Mungu anaweza kutoa jambo zuri ndani yako na ukawaaibisha watesaji.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.