TAMASHA LA USIKU WA AMANI KATIKA PICHA KUTOKA KARATU


Usiku wa Amani ni jina lililopewa tamasha la usiku wa kumsifu na kumtukuza Mungu. Na Awamu hii, Karatu ndio wamekuwa wenyeji wa tamasha hili ambalo limefanyika kwenye ukumbu wa Wakorea, kama ambavyo limeandaliwa na Habari Maalum. Media.

Tofauti sana na ilivyozoelekwa, watu waliweza kumsifu Mungu wakiongozwa na kikosi cha Rhema Worship Team ambacho kilitumiwa vilivyo na Roho Mtakatifu hata kupelekea watu kufunguliwa, na wengine wakipata huduma ya maombi kutoka kwa wachungjai mbalimbali waliokuwepo usiku huo.

Kwaya na waimbaji binafsi kutoka Karatu na Arusha wamehudumu usiku huo, akiwepo Ester Yohana, Jenipher Sita, Mnene Makweta na B Zablon.

Gospel Kitaa nayo iliweza kuweka kambi katika Tamasha hilo na hizi ni baadhi ya picha kama tulivyokukusanyia.


Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.