WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU

Sehemu ya kusanbyiko la watoto wakimsikiliza Uncle D.
Katika kundi la watoto, likauzlizwa swali, "wangapi huwa wanakula sadaka?" Kisha mikono kadhaa ikaenda hewani... ukiona hilo jambo basi ujue kwanza kuna safari ndefu, na pili inafariji.

Mosi, kuna safari ndefu kwa maana wanyooshao mikono ni wawakilishi tu kati ya wengi dunia nzima ambao hupewa sadaka na kuishia kula 'askirimu', ubuyu na hata mabungo, halikadhalika sambusa na eggchop.

 
Pili inafariji maana mikono mingi yamaanisha watoto ni waaminifu, na wanahitaji kuelekezwa na kukumbushwa njia iwafaayo, Na haya ndio yaliyojiri Moshi kwenye kusanyiko lililoandaliwa na Fountain Radio chini ya uratibu wa Uncle D (Desdery Charles Hotay Mtoto wa Madhabahuni), kusudi wapate kusemezana.

Maadili ya mtoto, Kujitambua kwa mtoto, na kujiamini ni sehemu ya mambo ambayo yamenuiwa. Lakini pamoja na hayo, kusanyiko hili lililowapa faraja watoto Mjini Moshi, limefanikisha kutambua kwamba kuna kundi miongoni mwa haohao watoto, ambao wameachwa nyuma, na hasa wale ambao hawalelewi kiroho. Hivyo kuwawekea msingi kama huu kutawafanya kuwa chini ya madhabahu ya Mungu na kumtumikia.

Kwa ujumla, kusanyiko hili la kwanza lilipata watoto takribani mia tatu, na huo ndio wmanzo wake tu, endelea kufuatilia GK nayo itakufahamisha hatua kwa hatua ikiwemo mkakati wa kusanyiko lijali ambalo litakuwa na utukufu maradufu. Na muda huo ufikapo, usiwe chukizo mbele za Mungu kwa kuwazuia watoto kama ambavyo wanafunzi walijaribu (Marko 10:13-14) - bali ufanyike furaha maana ufalme

Zifuatazo ni picha za tukio hilo lililofanyika katika uwanja wa Fountain Radio 95.7 FM, Mjini Moshi, tarehe 15 Mei 2016.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.