WORSHIP HOUSE WAZURU NCHINI MAREKANIKundi maarufu la injili la Worship House kutoka Limpopo Afrika ya kusini, limeondoka jana kuelekea nchini Marekani ambako limepata mwaliko wa kihuduma. Kundi hilo limeondoka na baadhi ya waimbaji wake kwa kutumia usafiri wa shirika la ndege la Emirates na kwamba litakuwa nchini Marekani kwa siku kadhaa kabla ya kurejea Afrika ya kusini tayari kujiandaa kurekodi DVD yao ya 13.

Worship House ni moja kati ya makundi yaliyojizolea mashabiki na tuzo mbalimbali nchini Afrika ya kusini kutokana na uimbaji wao, huku nyimbo nyingi za kitamaduni ama kitabuni ambazo huimbwa na watu mbalimbali nchini humo, huwa kundi hilo huimba kwanza na kurekodi ndipo Joyous Celebration hurekodi tena kwa ubora zaidi, ingawa haimaanishi kwamba JC huwa wanaiga kutoka katika kundi hilo.


"Lost without You"kutoka katika DVD no 7 yao Worship HouseShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.