AFRIKA YAZIDI KUJIUNGA BAADA YA KUZINDUA HATI MOJA YA KUSAFIRIA

Ile mipaka iliyowekwa miaka mingi iliyopita, kutenganisha kwa mistari iliyonyooka katika kujigawia rasilimali kwa wakoloni sasa inaelekea kuzidi kupanguliwa baada ya Umoja wa Afrika (AU) kuzindua hati ya kusafiria kwa Waafrika, katika mkutano wa mataifa hayo unaoendelea nchini Rwanda.
Rais Kagame na Rais Idris Deby wa Chad ©BBC

Rais Paul Kagame ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo, ndiye mtu wa kwanza kukabidhiwa hati hiyo pamoja na Rais Deby wa Chad, ambayo itawawezesha kutembelea nchi zozote zile kama Waafrika, na si kutambuliwa kwa mataifa wanayotokea.

Kwa hivi sasa hati za kusafiria zilizotolewa ni za kidiplomasia, na inatarajiwa kwamba hadi kufikia mwaka 2018 wakazi wa bara hili wataanza kumiliki hati hizi.

Mkutano wa Berlin (1884-1885) ndio ulioweka mipaka ya sasa kuigawa Afrika. ©Slide Bean
Hadi kufikia sasa ni taifa la Rwanda pekee ambalo Muafrika yeyote anaweza kuingia bila kuhitaji kibali (visa). Hatua hiyo ilichangia kukua kwa uchumi wake maradufu, na utekelezaji wa uwepo wa passport za aina moja kwa bara zima la Afrika huenda ukasaidia ukuaji wa uchumi na kupunguza uhamiaji haramu.

Muonekano wa hati za kusafiria za kidiplomasia za Afrika ©BBCShare on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.