CHAGUO LA GK WIMBO KUTOKA KWA MAGWIJI WA MUZIKI WA INJILI NCHINI CONGOWimbo ambao tumekuchagulia siku ya leo ni Asifiwe, utunzi wake gwiji wa muziki wa injili nchini Congo marehemu Charles Mombaya ambaye pia ndiye aliyeanzisha wimbo huu, katika video iliyopewa jina la wimbo huu akiwa amewashirikisha waimbaji nyota wa muziki wa injili nchini Zaire wakati huo sasa hivi ni Jamhuri ya Demokrasia Congo.

Wimbo huu wa kuabudu umetokea kupendwa na wengi hasa namna sauti zilivyopangiliwa sambamba na ujumbe upatikanao ndani yake. Charles Mombaya alikuwa mwimbaji na mwanamuziki wa injili aliyewaunganisha waimbaji wengi wa injili nchini humo ikiwa sambamba na kuwawezesha kurekodi nyimbo zao kupitia studio yake.. Amefariki takribani miaka 20 iliyopita. Tunakutakia utazamaji mwema wa wimbo huu na Jumapili njema


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.