HIVI PUNDE: JOYOUS 21 KUREKODIWA MAREKANI KWA T.D JAKES

Sehemu ya wapigaji Joyous20 Jijini Durban, ambayo GK ilihudhuria. (Picha zaidi)
Habari za hivi punde ambazo zimeifikia Gospel Kitaa zinaeleza kwamba ni rasmi albamu ya 21 ya kundi la Joyous Celebration itarekodiwa Potters House, kanisa linaloongozwa na Askofu T.D Jakes, lililopo Dallas.
video
Askofu Jakes akivunja ukimywa kwa waumini wake kuhusiana na ujio wa Joyous Celebration, na hapa akiwafafanulia waumini wake kwamba ni kama vile Beyoncé akubalikavyo nchini Marekani. Katika kuleta ulinganisho.


Habari hizi ambazo zimethibitishwa kwenye ibada ya leo nchini Marekani, ambapo Askofu Jakes ameeleza kwamba kundi hilo litafany alive recording kwa kushirikiana na kwaya wenyeji ya kanisa hilo.

Habari hizi zilizo njema kwa wadau wa muziki wa injili mahala pengi duniani hazijapokelewa vizuri na kila mtu, kwani baadhi ya mashabiki wameonyesha kusikitika na kwamba hali hiyo itawanyima fursa ya kuhudhuria tamasha hilo kwa kuwa ni gharama kusafiri, na lisha ya hivyo inaweza kupelekea nyimbo nyingi kuwa za Kiingereza badala ya lugha ya nyumbani.


BREAKING NEWS Bishop TD Jakes announces at his Sunday morning service in Dallas Texas that Joyous Celebration will...
Posted by MY Joyous Celebration on Sunday, 17 July 2016
Pamoja na waliolalamika, bado wengine wamefurahia zaidi na kuitaka Joyous ifike mbali zaidi katika kuhubiri injili kwa mataifa. Endelea kufuatilia GK nasi tutakufahamisha zaidi kuhusiana na habari hizi.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.