SOMO: SIKUWAMBIA ITAKUWA RAHISI - MCHUNGAJI KILIMA
SOMO: SIKUWAMBIA ITAKUWA RAHISI
Na: Mchungaji John Kilima

Joshua 1:1-
Joshua naye alikuwa mpiganaji, aliwahi kupigana na Waamaleki hivyo alikuwa hodari. Nchi ambayo walikuwa wanaenda kuimiliki wana wa Israel tayari ilikuwa ina mataifa yanaishi, wahiti, waahivi, wayebusi, wakaanani na waamori.

Haiwezi kuwa rahisi katika kuifikia nchi ya ahadi lakini Mungu atakuwa pamoja nawe kwani amesema “sitakuacha wala kukupungukia”.
Meshaki na wenzie waliwekwa katika tanuru la moto lakini Mungu akawa pamoja nao katikati ya moto huo akaonekana kama mtu wanne hivyo wakawa katikati ya moto lakini salama.
Utajuaje Mungu yuko pamoja nawe?

Mungu ni neno na neno ni Mungu. Neno(Mungu) linasema kaeni katika neno. Mungu huangalia neno apate kulitimiza ndio maana ni vizuri kuweka neno la Mungu moyoni mwako……neno lako nimeliweka moyoni mwangu nisije nikakutenda dhambi.mkikaa katika neno langu ombeni lolote kwa Jina langu nami nitawapa. Mungu yuko katika neno lake ukiwa na neno la Mungu utavuka popote pale.

Kama huna neno la Mungu ni hatari sana hata kutenda dhambi inakuwa rahisi kwani hautakuwa na neno la kukuonya usitende dhambi. Mkikaa katika neno langumtakuwa huru kwelikweli.
Ipo kazi katika kuutafuta uhuru wa kweli. Wana wa Israeli baada ya kuvuka bahari ya shamu wakakumbuka vitu vya Misri wakaona kuwa Misri ndio walikuwa huru kuliko kwenye jangwa walilopitia na kuanza kumlaumu Musa kwamba ni heri angewaacha wakafikia misri kuliko jangwani walipo. Kuna shida na mateso, mateso humtengeneza mtu ili awe wa tofauti katika kazi ya Mungu hata utakapokuwa huru utajua ni kweli umekuwa huru kwelikweli kwa neno lake.
Zaburi 126:4-6
Wapandao kwa machozi watavuna kwa furaha. Wana wa Israel walipanda kwa machozi kwa kuwatoa wale mataifa matano ili watakapokuwa wakinywa maziwa na asali wanywe kwa furaha. Shida yako unataka kupanda kwa furaha ndio maana unapokutana na jambo gumu unakata tamaa kwa haraka.
Wokovu ni vita na wala si tambarare kama wengi wanavyofikiri. Paulo pamoja na kuwa ameandika vitabu vingi lakini alizuiliwa mara nyingi na shetani. Si rahisi kuimiliki vitu ambavyo tayari vilikuwa vinamilikiwa lakini kwakuwa Mungu amesema basi itakuwa na pia amesema tumejengwa juu ya mwamba na malango ya kuzimu hayatatushinda hivyo kumiliki ni lazima.

Mungu anapenda mtu mpiganaji, ndio maana aliacha mataifa matano ili watakaozaliwa nao wajifunze vita. Ahadi ya mtu ipo kwenye maumivu ndio maana mtu hupanda kwa machozi, umekaa kwa muda mrefu hujapata mtoto, kazi, mume/mke lazima upande kwa machozi ili uvune kwa kicheko. Mtoto ni Baraka lakini anapatikana kwa uchungu.
Isaya56:
Siku ya mavuno huwa ni kicheko na kelele. Watu hawapandi kwa furaha siku zote wanapanda kwa machozi mateso yanapozidi ndivyo Baraka inavyokaribia kuzaliwa
Isaya37:1-
Siku zote shetani akiona kile unachokuwa unakitafuta kinakaribia ndivyo vita inavyozidi kuwa kubwa. Baraka ya mtoto inamfanya mtu asahau uchungu wote. Ndivyo nawe utakavyofurahia pindi utakapopata kile unachokitafuta. Hebu angalia alichokisema Isaya kwa Hezekia.
Isaya 37:3
Mungu amewaandaa wao ili kukufanya wewe usonge mbele vitani. Mungu akiondoa vita yote kwako, hutakesha, hutafunga na pia hutahudhuria ibada. Ndio maana Mungu akayaacha mataifa matano ili wajifunze vita wamtafute Mungu nawe katika maisha yako ya wokovu tegemea vita na wala si wokovu tambarare lakini utashinda ukiamua kipambana kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.

MAOMBI:
Kwa damu ya Yesu navipanga vita kusambaratisha mawakala wote wa giza waliotumwa kunizuia nisiingie kwenye Baraka yangu, naachilia moto kuwaangamiza wote, sitazuiwa na chochote kwa damu ya Yesu. Mliotumwa kunipinga nawapinga kwa damu ya Yesu mmekuja kwa njia moja nawatawanya kwa njia saba. Wajumbe wa kuzimu waliovaa sura ya ndugu, au rafiki au mtu awaye yote ili kunizuia nakusambaratisha kw aJina la Yesu, nakutawanya ewe mlima mrefu uliotumwa kunizuia . nanyamazisha damu zote zilizomwagika kwemye madhabahu za giza ili kunifanya nisipige hatua natumia damua ya Yesu kunyamazisha damu zote maana imeandikwa nao wakamshinda kwa damu ya Yesu.

AMEN
INFORMATION AND MEDIA MINISTRY
UFUFUO NA UZIMA –TANGA.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.