TANZIA KWA KWAYA MAARUFU NCHINI WAIMBAJI WAKE WAKONGWE WATATU WAAGA DUNIA

Marehemu Charles Sokoro wa AIC Makongoro choir Mwanza
Wiki iliyoisha imeacha majonzi kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini baada ya waimbaji na wapigaji watatu kutoka kwaya tofauti wameitwa kutoka katika ulimwengu huu. Waimbaji ambao wameripotiwa kufariki ni pamoja na aliyekuwa mwalimu na mpigaji wa kwaya kongwe nchini ya AIC Makongoro Mwanza waliotamba enzi hizo na nyimbo kama 'Wana Israel' marehemu Charles Sokoro.

Mzee Semangembe wa Mamajusi Choir Majengo Moshi
Mwingine ni mzee Semangembemwimbaji wa kwaya ya Mamajusi ya kanisa Anglikana Majengo Moshi, na hapo jana usiku kwaya kongwe ya Tumaini Shangilieni Arusha ilimpoteza mwimbaji mwenzao wa siku nyingi mama Veronica Sepeku aliyefariki kwa ajali ya kugongwa na gari usiku wa kuamkia leo.

Marehemu Veronica wa kwanza upande wa kulia

Marehemu Veronica Sepeku

Gospel Kitaa inawapa pole wale wote waliofikwa na misiba hii, zaidi kila mmoja wetu ajihoji ndani yake ya kwamba jina lako likiitwa leo hii mbinguni je utakuwa tayari?

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE 


Tafakari kupitia ujumbe huu wa waimbaji wa Tumaini Shangilieni Choir Arusha


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.