TAZAMA VIWANGO VYA JUU KATIKA KUMSIFU MUNGU NDANI YA CHAGUO LA GK

Mchungaji Khaya Mthethwa
Katika chaguo la GK leo tupo Afrika ya kusini tumekuchagulia kati ya kazi mpya kabisa kutolewa na mmoja kati ya waimbaji waliopata mafanikio ya haraka katika medani ya muziki wa injili nchini humo kijana Khaya Mthethwa ambaye ni mshindi wa SA Idols mwaka juzi lakini pia akiwa mmoja wa waimbaji waliosukwa vyema na kundi la Joyous Celebration. 

Hivi karibuni aliachia DVD yake mpya kabisa ya kwanza aliyofanya live iitwayo 'The Dawn'. Ndani ya DVD hii kuna nyimbo nyingi ikiwemo Simi Lapha remix iliyotungwa na Ntokozo Mbambo na ndio chaguo tulilokuchagulia siku ya leo.  Licha ya kwamba Ntokozo aliimba wimbo huu kwa mara ya kwanza kwenye DVD yake ya kwanza kisha kurekodi tena katika DVD yake ya pili iitwayo 'Filled' aliamua kuutengeneza tena wimbo huu na kumpatia Khaya akiwa ameshirikishwa kuuimba pia. Tunakutakia utazamaji mwema wa wimbo huu. Mungu akubariki

Ntokozo Mbambo akiimba katika recording yake Khaya
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.