ULINIUMBA NIKUABUDU NDIO CHAGUO LA GK, UTUMISHI ULIOTUKUKA WAKE CHIBALONZA

Marehemu Angela Chibalonza Muliri enzi za uhai wake katika huduma ©niaje

Katika chaguo la GK hii leo, tunakuletea moja ya nyimbo zilizomtambulisha vyema mwanamuziki na mwinjilisti kwa upande wa uimbaji marehemu Angela Chibalonza wa Muliri uitwao 'Uliniumba Nikuabudu' aliyefariki dunia kwa ajali ya gari miaka 9 iliyopita jijini Nairobi nchini Kenya ambako ndiko kulikokuwa makazi yake.

Angela alitokea kuwa kipenzi cha mtu yeyote yule aliyebahatika kusikia kazi zake licha ya kutoa album nyingine kabla ya hii lakini kwa upande wa Tanzania alianza kuvuma kupitia album hii iliyohusisha wimbo huu wa 'Uliniumba Nikuabudu'. Licha ya kutokuwepo katika ulimwengu huu kwasasa, lakini bado kazi zake njema na nzuri zinaendelea kubariki na kufungua mioyo ya watu waliowengi sehemu mbalimbali duniani. Tukutakie baraka za Mungu utazamapo wimbo huu

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.