USHUHUDA: IMANI YAMPONYA UGONJWA WA SARATANI

©YouTube Screengrab
Hakika Neno litasimama, mambo yote yatapita lakini neno litasimama. Ushuhuda huu ni wa mwanamama mmoja aliyepata uponyaji wa ugonjwa wa saratani ambao ulikuwa umemfika ukingoni na hata kusalimu amri ya kwamba amekaribia kuaga dunia.

Mwanamama huyu anatukumbusha ya kwamba mahitaji yetu hata yawe makubwa kiasi gani, bado kwa Mungu yote yanawezekana na tukishikilia imani kama ilivyoandikwa kwenye Kitabu cha Mathayo 21:21

"Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea

Licha ya kuwa kwenye hatua ya kushindwa kutembea mwenyewe na hata kushindwa kunyanya pochi yake mwenye kwa mkono wake wa kushoto, na pamoja na daktari kumuarifu kuwa hana muda mrefu wa kuishi kulingana na vipimo vilivyoonyesha uvimbe kwenye mifupa yake, bado hakukata tamaa na kuamua kwenda kuhudhuria mkutano wa injili nchini Singapore, ambapo alipokea muujiza wake, na sasa akishuhudia ulimwengu.

Kilichojiri
Akiwa kwenye mkutano huo wa injili, muhubiri alianza kutaja watu wenye magonjwa mbalimbali akiwafahamisha kwamba Yesu anataka awaponye. Lakini mwanamama huyu aliamua hatoenda mbele hadi pale watakapotaja ugonjwa wake mahsusi hivyo aliamua kutulia kwenye nafasi yake tu akiomba Mungu hilo litokee.

Baada ya kitambo kidogo mhubiri aligeukia upande wake na kusema kwamba kuna mtu anasumbuliwa na uvimbe kwenye mifupa na Yesu atamponya, jambo hilo lilimstua na kutambua kwamba mlengwa ni yeye. Kwa maumivu akaanza kusimama huku akiwaza ni namna gani atafika mbele kwenye umati wa watu takriban elfu nane. wasaidizi wake walikuwa pembeni yake ili kumlida asiguswe na mtu akaanguka, kwa maana alikuwa dhaifu.

Lakini ghafla akahisi kama kuna tofauti, kisha akajaribu kuinua pochi yake kwa mkono wake wa kushoto, jambo ambalo alikuwa hawezi kufanya. Ikamshangaza kuona kwamba anaweza kuinua hiyo pochi. Kisha akajaribu kama kutembea mwenyewe, ikamshangaza zaidi ya kwamba ameweza. Kilichofuata ni kujaribu kuinua mikono juu na hata kugeuka nyuma kutazama waliopo, nalo akaweza. Ndiposa akatambua ya kwamba uponyaji umeshaanza kufanya kazi.

Baada ya kurudi nyumbani kwake ilibidi akamfate daktari wake na kumueleza yaliyojiri, na kwamba ni Yesu tu ailyemponya, daktari akibaki anashangaa na kusadiki. Ufuatao ni ushuhuda wake mwanamama huyu kama ambavyo ameutoa kwenye kanisa la Bethel, Redding, California nchini Marekani.

Nawe hapo ulipo usitazame ukubwa wa tatizo lako, tazama ukubwa wa Jina la Yesu, ambaye adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake. Na kwa kupigwa kwake, sisi tumepona. Uwe na siku njema yenye matumaini mapya.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.