WAUZA CD FEKI WAPEWA SIKU 30 KUACHA BIASHARA ZAO

Maafisa usalama pamoja na Msama katika moja ya oparesheni mwaka 2014 ©Michuzi Matukio Blog
Mwezi mmoja umetolewa kwa ajili ya usitishwaji wa kuuza kazi feki za wasanii mbalimbali hapa nchini, ikiwa ni moja ya chanzo cha kupoteza mapato kwa wenye kazi hizo - huku wanaofaidikia wakifanya hivyo kwa njia ambayo ni haramu.

Akizungumza kuhusu hilo Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wezi wa kazi za sanaa wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo husika, amesema baada ya siku 30 watawashukia wafanyabiashara hao wasio waaminifu.

“Tunatoa siku 30 kwa wanaofanya biashara ya kazi feki za wasanii, hiyo biashara waachane nayo kwa sababu inapoteza pato la Taifa,” alisema Msama.

Msama alisema kwa kuanzia watapita nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na mkoa kwa mkoa ili kusaka computer zinazotumika kuiba kazi za sanaa.

Jeshi la Polisi ni chombo ambacho pia kinahusika kwenye oparesheni hii, ikiwemo Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo sambamba na kwa lengo la kusafisha tatizo hilo.

Aidha Msama alisema ili kukomesha zoezi hilo wakikuta kazi feki kwenye duka wanabeba mzigo mzima wa kazi za sanaa.

Naye Inspekta Jenera wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu alisema jamii inatakiwa kutoa ushirikiano na Polisi katika jambo hilo ambalo linaumiza nguvu kazi ya Taifa.

IGP Mangu alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa Polisi ili kazi ifanyike inavyotakiwa kwa lengo la maendeleo ya wasanii ambao wanasaka namna ya kuendeleza maisha yao.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.