BAADA YA KARIBU NDANI YANGU, LIVE RECORDING MARTHA UHWELLO DISEMBA 2016

Martha Uhwello.
Kwa takribani miaka mitatu ibada ya kusifu na kuabudu imekuwa likipangwa bila kufanyika, sababu kadha wa kadha zikipelekea ikiwemo za kuhuzunisha na za kufurahisha pamoja na changamoto za kiutawala. Lakini hatimaye mwaka huu 2016 pamoja na kuimba na VOT, jambo lililokuwa linakereketa ndani ya  Martha Uhwello likatimia.

Karibu Ndani Yangu ni tukio la kwanza ambalo limeadaliwa na Martha, lengo kubwa ikiwa ni ibada na utamblisho wa Martha kama Martha katika huduma. Hilo Likafanikiwa. Na hatimaye njia imefunguka kuelekea Disemba, live recording.

Tukio hilo ambalo limefanyika kwenye kanisa la EAGT Elerai almaarufu kama Bonde la Baraka kwa Mchungaji Marko Haule, lilianza mida ya saa tisa alasiri, ambapo wakazi waliofika eneo hilo walitoka wakiwa tofauti.

Ibada za kusifu na kuabudu zitakuwepo kama kawaida, na shauku kubwa ya Martha ni kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Uwepo wa ibada zenye ujazo wa Roho Mtakatifu hasa ndo shauku kubwa.

Kati ya watoto watatu, yeye ndiye pekee wa kike, na ni mtoto wa Mchungaji Deogratius Uhwello ambaye pia huimba na kupiga vyombo. Pamoja na kurithi uimbaji lakini pia amenolewa chini ya Mwalimu Barnabas Philip, kabla ya kulelewa zaidi na Voice of Triumph (Shangwe Voices).

Arusha, kama inavyofahamika kwa jina la The City of Praise (Jiji lenye kumsifu Mungu), lilikutanisha wahudumu mbalimbali katika Injili kama vile CAHOGO'z, Efraa Musica, FDG, na wengine wengi.

Zifuatazo ni picha za tukio hilo la tarehe 17 Julai 2016.

Mchungaji MC Barnabas Philip
Rais wa Shangwe Voices Elder Tolla'g
Abednego & The Worshippers
Chief Pianist Jimmy Kimutuo

Baba na Mama Mchungaji Barnabas Philip
Timu ya Martha; Eva Doxa, Careecious Massawe, Hannah Kimaro, Furaha Loi, Imma Canna, na Nuru Masunga

Sehemu ya umati


Mchungaji Marko Haule
Na kama ulikuwa hujui, basi jina la karibu Ndani Yangu limepatikana kupitia njozi baada ya kufanya maombi. Na timu ya wote uwaonao na hata usiowaona, ndio iliyofanikisha siku kutimia kwa utukufu wa Mungu.

Na hao wote Martha anaeleza kuwashukuru sana, na kwamba kilichopo sasa ni kulinda moyo wa ibada na kuishi maisha ya ibada - "hata pale Mungu anapokuinua, usilewe sifa" Mungu huangalia roho.

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.