EWE MJUSI, UMEFATA NINI NYUMA YA MLANGO

Elie Chansa.
Staff Writer.
©King of Wallpapers
Ni dhahiri kwamba nyumba ni pana na inatosha kwa mizunguko na mawindo yako, angalau ukifika kona moja unweza kumkamata inzi. Ama ukiwa kwenye kona mojawapo unaweza pia kuhemea wadudu wadogo wadogo na maisha yakasonga.

Lakini kitu nisichoelewa ni pale unapopendelea kukaa nyuma ya mlango. Unafanya nini huko ilhali unajua kwamba ni sehemu hatari kwa maisha yako?

Hivi hukumbuki hata msemo umetungwa ni kwa sababu yako kupenda kukaa huko? “Unatoa macho kama mjusi kabanwa na mlango”. Kana kwamba haitoshi, bado ukaendelea kukaa huko ili macho yakutoke pima.

Mwenzako alienda huko, kilichomkuta ni historia, alibanwa na akasahaulika – maisha yakaendelea mbele kama kawaida. Nawe sasa ukaona ukafanye utafiti ni kitu gani kiko huko, bila kutambua kwamba mlango utafungwa muda wowote nawe utakuwa historia.

Mlango unapofungwa hakuna anaeangalia kama wewe mjusi umekaa huko, hakuna anayejali kama uko kwenye mkakati wa kupunguza inzi ndani ya nyumba. Ukibanwa ndo hivyo kwisha habari yako, na hata mayai yako hutashuhudia yakitotoka na kupata kizazi kingine.

Nakumbuka ulikuwa na nguvu ya kuruka hapa na pale katika kusaka mlo wa kila siku, na hilo jambo uliliweza. Ngozi yako iliyofanana rangi na ukuta ilikupa uwezo wa kumnyemelea adui wako. Lakini haya yote kwa sasa hayahesabiki, maana wewe ni historia.

Haya yote mjusi umejisababishia. Umebaki mfano wa kutoigwa.
Nyuma ya mlango hapakufai, kaa eneo la wazi, na hakuna atakayekuwa na ugomvi nawe. Maisha yataendelea vema tu. Kama ukishindwa kusikia hiki, basi siku unaenda kukaa nyuma ya mlango, ndio itakuwa mwisho wako. Usimjaribu BWANA Mungu wako. Acha dhambi.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.