KAA TAYARI KUWASIKIA WANA DGC WAKIWA NA DVD MPYA HIVI KARIBUNIKama unajua uimbaji bora wa kwaya basi hapana shaka huwezi kukosa kuitaja moja ya kwaya inayofanya vyema kabisa katika kumtukuza Mungu kupitia waimbaji wake hodari na wapigaji, hawa si wengine bali ni Dar es salaam Gospel Choir (D.G.C) kutoka kanisa la Pentecoste kurasini jijini hapa.

Kama hujui ni kwamba kwaya hii ipo katika mchakato wa kumalizia kurekodi video yao mpya kabisa ambayo itakuwa ni toleo la nne. Tayari wameshamaliza kurekodi nyimbo kadhaa na kwamba zoezi hilo lipo ukingoni kabla haijatayarishwa na tayari kutolewa kwa wapenzi wa muziki wa injili kupata ujumbe wa Mungu kupitia waimbaji hao.

DGC wanasifika kwakuwa na waimbishaji wengi ama solo ambao wapo kwenye viwango lakini pia muziki na uimbaji wao kwa ujumla umefanyika baraka kwa wengi. Kama wewe ni mpenzi wa kwaya ama muziki wa injili na hauna matoleo ya kwaya hii, basi jiulize vizuri...Kaa tayari kupokea kutoka kwao DGC.

Angalia baadhi ya nyimbo wakati wakiendelea na kurekodi toleo jipya hivi karibuni

Tazama wimbo kutoka katika DVD yao ya pili

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.