MARIDHIANO NI MUHIMU KUELEKEA SEPTEMBA MOSI: ASKOFU GWAJIMA


Akizungumza wakati akihojiwa na kituo cha Television cha Star TV Askofu Dkt Josephat Gwajima amesema, "kuhusu mgogoro wa polisi na vyama vya siasa busara inahitajika, kwasababu vyama vya siasa vipo kisheria basi Jeshi la polisi lipate muda wa kuwasikiliza ili kulinda amani ya nchi maana hakuna haja ya kuhatarisha amani bila sababu"

Kuhusu kuenzi amani, amesema, " amani ni maliighafi mama kwa uchumi na ukuaji wa hali ya nchi yoyote, hivyo kuitunza amani ni kitu cha muhimu kuliko vyote kwasababu bila amani hakuna kuhubiri injili, wala hakuna ujenzi wa uchumi"

Aidha Askofu Gwajima amezungumzia mgogoro baina ya serikali na upinzani, na kueleza kwamba ni mazungumzo yakawepo ili kuridhiana kuliko kuishia kupigana ambapo madhara yake hufika hata kwa wasiohusika.

Chanzo: Star TV
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.