MKHULULI AKARIBISHWA RASMI TANZANIA, TAMASHA 28 JUMAPILI HII AICC


Hatimaye katika kuelekea siku ya tamasha la kusifu na kuabudu tarehe 28 kwenye ukumbi wa Simba, AICC Jijini Arusha. Mhudumu kiongozi wa tamasha hilo kutoka Afrika Kusini Mkhululi Bhebhe amekaribishwa rasmi nchini Tanzania katika tafrija fupi iliyofanyika Milestone Park, iliyopo Sakina.

Katika tafrija hii iliyoandaliwa na Abednego & The Worshippers Internationall kwa lengo la kumkaribisha Mkhululi Bhebhe nchini ilihusisha watu mbali mbali wakiwemo waandaaji wa tamasha hili la Arusha lets Praise pamoja na Abednego & The Worshippers International kwa lengo kuu la kutengeza njia, ukaribu na mwasiliano ya karibu kabisa kati ya Abednego & The Worshippers Intl pamoja na waimbaji wa nyimbo za injili katika nchi yetu ya Tanzania hadi  nchini Afrika Kusini.

Na pia katika keki na iliyoandaliwa na Abednego & The Worshippers International mahususi kabisa kwa kuonyesha upendo kwa Mkhululi Bhebhe kutokana na namna walivyofanya naye mazoezi kwa kipindi cha muda mfupi walioutumia pamoja na wanamuziki wao.


Tukutane siku ya Jumapili tarehe 28 mwezi wa nane 2016 pale AICC katika Ukumbi wa Simba.
GK tuatakuwepo kukuletea tukio zima.

Unagana nasi katika picha za tafrija pamoja za mazoezi yalifanyika katika kanisa la St.James Kaloleni.

Mkhululi Bhebhe akikabidhiwa keki Mkhululi Bhebhe Akiwa na Mkurugenzi wa Wz Intl

 
Hapo ni bada ya kula kipande cha Keki
Mkhululi na Misericordias

Music Director wa Wz International Nelson Mugarula (Nelly Music) 


Picha ya Pamoja Baada ya tafrija kumalizika


Mkhululi Bhebhe akiongea pamoja na kutoa shukrani zake za dhati kwa Abednego & The Worshippers Intl     


Kwa picha zaidi Bofya hapa >>


Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.