NYOTA WA MUZIKI WA INJILI AAMUA KUINGIA MAZIMA KWENYE FANI YA UCHEKESHAJIMwimbaji nyota anayesifika kwa kuwa na sauti nzuri ya tatu nchini Afrika ya kusini aitwaye Thembinkosi Manqele ameamua kupiga hatua kubwa zaidi katika fani yake ya uchekeshaji mara baada ya kuwataka marafiki na mashabiki wake wakae tayari kupokea kitu kipya kutoka kwake hivi karibuni.

Manqele ambaye amejipa jina la Mr Ministry katika uchekeshaji wake, ni mmoja kati ya waimbaji wanaotumiwa na waimbaji wengi afrika ya kusini kila wanaporekodi kanda zao, wakiwemo kama Ntokozo na mumewe Nqubeko, Khaya, Judith Sephuma na wengineo huku pia akiwa ni kaka wa kijana Sipho Manqele ambaye ni mume wa mwimbaji Mercy Ndlovu wote wakiwa wamewahi kuimbia Joyous Celebration.

Thembi na mkewe wakiwa katika pozi
Kwa kawaida mwimbaji huyu huwa anajirekodi video fupi za kuchekesha na kuweka katika kurasa yake ya Facebook na kutokea kupendwa na waliowengi wakiwemo wanamuziki. Ambapo hapo jana alienda mbali zaidi kwa kupiga picha aina mbili moja akiwa amevalia kama mwanamke na nyingine akiwa amevaa kawaida na kuziwekea maneno kwamba kutana na mama maNjongo na baba kam Mdu, na kusema kwamba anahamu kuwatambulisha marafiki zake kazi yake mpya itakayotoka hivi karibuni. Picha hiyo imepokelewa kwa vicheko na watu wakionyesha kukaa tayari kuona hiyo kazi mpya.

Picha aliyoiweka kutangaza ujio wa kazi yake mpya
Tembinkosi ni baba wa mtoto mmoja na mke mmoja na mwimbaji maridadi wa sauti ya tatu ambaye unaweza kumuona katika DVD za waimbaji wengi wa Afrika ya kusini akishiriki katika kusukuma sauti ya tatu.Video za vichekesho vyake unaweza kuviona kupitia YouTube akiwa ameigiza kwa lugha ya kwao pia vichache kwa kiingereza.

Tazama moja ya vichekesho vyake akiigiza mambo ya wahubiri

Tazama ubora wa sauti yake akiimba He lifted me Up akiwa kwenye kipindi cha Gospel Classic


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.