NYOTA WA MUZIKI WA INJILI KATIKA MAPAMBANO NA MASHABIKI WAKIMKATAZA KUCHORA TATTOO MWILININyota wa muziki nchini Afrika ya kusini ambaye pia ni mchungaji wa moja ya kanisa nchini humo kijana Khaya Mthethwa ambaye alikuwa mshindi wa shindano la SA Idol mwaka juzi pia amewahi kuwa mwimbaji wa Joyous Celebration, amejikuta katika mapambano na mashabiki pamoja na rafiki zake katika Facebook baada ya mwimbaji huyo alipoandika kwamba anataka kujichora tattoo na kuacha swali kwamba ndio au hapana, ambapo alipata upinzani mkali wakipinga asijichore tattoo

Khaya ambaye alikuwa matembezini jijini New York nchini Marekani kwa takribani wiki tatu, aliweza kuwajibu na kuwauliza maswali watu hao ambao wengine walidai kujichora ni dhambi kama Mungu aliona inapendeza basi angewafanya magazeti ili wajichore lakini haikuwa hivyo, kitendo ambacho pia mwimbaji huyo anayetamba na DVD yake mpya ya The Uprising New Dawn kuwauliza kama ni hivyo kwanini nawao wadada wanavaa hereni na mapambo mengine kwakuwa yeye pia anajua kwamba kujichora ni mojawapo ya kutunza mwili wake kwa utukufu wa Mungu
Aidha mwimbaji huyo amekuwa akiandamwa kwa habari ambazo yeye mwenyewe amekanusha na hajui zilikoanzia kuhusiana na safari yake hiyo ya nchini Marekani ikiwa ni mara yake ya kwanza, ambapo gazeti maarufu la udaku nchini humo la dailysun na vyombo vingine vimeandika kwamba mwimbaji huyo alifukuzwa hotelini kwa kosa la kutembea pekupeku bila kuvaa viatu jambo ambalo limemfanya mwimbaji huyo kucheka na kuweka maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook ambako mashabiki wake wamekuwa wakishangaa kwajinsi gazeti hilo linavyomwandama kwa habari za uongo.


Settle for Less kutoka kwa Khaya 


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.