PASTOR DUBE AENDELEA KUONYESHA UKONGWE WAKE KATIKA MUZIKI WA INJILI

Pastor Dube akikabidhiwa uthibitisho wa album yake kufikia kiwango cha Gold
Mwimbaji mkongwe anayefanya vizuri kwenye muziki wa injili ndani na nje ya bara la Afrika Pastor Benjamin Dube ameendelea kupata mafanikio katika medani hiyo, baada ya hivi karibuni album yake mpya aliyoitoa mapema mwezi September mwaka jana imefikia kiwango cha dhahabu ama Gold kwenye mauzo yake.

Album hiyo 'Sanctified In His Presence' ambayo ilirekodiwa kwenye ukumbi wa Carnival City Top
Pastor Dube na wanawe
Arena, kwa mara ya kwanza mbele ya umati wa watu tofauti na alivyozoea kurekodi album zake zilizopita, safari hii aliyekuwa amemkabidhi kazi ya kuongoza muziki ama music director alikuwa kijana aliyebarikiwa kwenye muziki Nqubeko Mbatha ambaye naye yupo mbioni kurekodi album yake mpya hivi karibuni.

Licha ya mafanikio kwa upande wa mauzo lakini pia album hiyo ilijinyakulia tuzo ya album bora ya injili kwenye tuzo za Sabc Crown Gospel Award zinazofanyika kila mwaka nchini Afrika ya kusini licha ya kwamba mkongwe huyo aliwahi kulalamika na kuwataka waandaaji wa tuzo hizo kuacha kumjumuisha katika tuzo hizo kutokana na kwamba alishawahi kukabidhiwa a life time achievement na hivyo kutaka kutojumishwa kwenye tuzo hizo kwakuwa haitakuwa busara kwa waimbaji wengine. Aidha hii si album ya kwanza ya Pastor Dube kufikia kiwango cha Gold katika mauzo ni mwendelezo wa kazi zake nyingi zilizopita ambazo nazo zilifikia kiwango hicho.
Baadhi ya picha za album zilizofikisha kiwango cha Gold za pastor Dube ambaye amesema kwasasa hana nafasi pa kuziweka kwakuwa ukuta wake umejaa baraka hizo


Tazama wimbo 'Lona Baratang' aliomshirikisha mwanadada Thandiwe ndani ya Sanctified 

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.