SOMO: KITABU CHA UKUMBUSHO CHA WANAOMTUMIKIA BWANA - ASKOFU GWAJIMA

Askofu Dkt Josephat Gwajima kanisa la Ufufuo na Uzima

“KITABU CHA UKUMBUSHO CHA WANAOMTUMIKIA BWANA”

Malaki 3: 12 “Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.”


Wafilipi 4: 3 “Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.”

Mtume Paulo anawaambia wafilipi wale waliotenda kazi pamoja naye kwamba majina yao yamo katika kitabu. Tunajifunza kwamba ukimtumikia Bwana jina lako linaandikwa kwenye kitabu cha Uzima.
Ufunuo wa Yohana 21: 27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.”

Watu wengi wanasema kumtumikia Mungu hakuna faida jambo ambalo sio kweli ni upotoshaji.
“Mungu anawasikiliza sana wale wanaomtumikia”
Malaki 3: 14 “Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi?”

Yoshua 22: 5 “Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa Bwana, aliwaamuru, kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.”

Kuenenda katika njia yake ni kumtumikia Bwana, kuinua mikono na kumwabudu ni kumtumikia Bwana kwa ufupi zipo nafasi nyingi za kumtumikia Mungu na mifano yake ipo kwenye Biblia. Mungu aliwatoa watu wake kutoka misri kwenda kwenye nchi ya Israeli Ili wamtumikie ndio maana alikuwa akimwambia Farao” awaache watu wangu waende wakamtumikie.”

Kitendo cha kuokoka kinafananishwa na kutoka kwenye nchi ya Misri ya utumwa kwenda Israeli nchi ya ahadi. Eliya alikuwa anamtumikia Mungu na alikuwa hajulikani ametoka wapi akatabiri akasema hakuna mvua itakayonyesha kwa muda wa zaidi ya miaka 3 na hakuna atakayeruhusu inyeshe bila yeye na ikawa hivyo. Huyu ndiye ambaye Mungu wake alidondosha mawe kutoka mbinguni yakawapiga adui za Israeli vitani, huyu ndiye ambaye Mungu wake aliigawa bahari ya shamu Israeli wakapita, huyu ndiye ambaye Mungu wake alisimamisha jua ili watu wake washinde vita. Mungu huyo ndiye ambaye sisi tunamtumikia ni Mungu mwenye kushika agano lake.

Kumbukumbu la torati 6: 13 “Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.”

Kumbukumbu la torati 10: 12 “Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?”

Watu wengi wanawaza ukisema kumtumikia Bwana uende chuo fulani cha Biblia ili ukasome kwa muda fulani ukitoka huko uanze kuvaa kofia za aina fulani ndipo uanze kumtumikia Mungu huko sio kumtumikia Bwana Mungu, wengine wanasema uanze seminari uende mpaka ukasome Italy upate elimu fulani ndipo uwe padiri ndio uitwe unamtumikia Mungu, Huko sio kumtumikia Mungu ni kuitumikia dini, mwangalie Petro alikwenda wapi kujifunza kumtumikia Mungu zaidi ya kukaa pamoja na Bwana Yesu na kuona kazi zote alizofanya, kujifunza mafundisho yake yote na baadaye alikuja kumtumikia Mungu kwa uwezo mkubwa bila kusoma elimu yeyote ile ya kidini, Danieli alikuwa mbunge lakini alimtuikia Mungu, Petro hakuwa na elimu yeyote ile ya kidunia lakini hilo halikumpa shida na hakuhangaika alikuwa anaijua Biblia ndiomaana alipomkuta Yule kilema kwenye lango alimwambia tazama sisi hatuna fedha wala dhahabu ila tulicho nacho ndicho tukupacho simama uende kwa jina la Yesu na Yule kilema akasimama akawa mzima.

Daniel 2: 48 “Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli. Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.”

Danieli alikuwa mbunge lakini alimtumikia Mungu, aliweza kufanya kazi ya Bwana na kazi ya serikali pamoja na kina shadrak, meshak, na Abednego walikuwa wakuu wa mikoa wote walikuwa wanamtumikia Mungu, walikuwa wanakaa pamoja na wageni wa nchi ile lakini hawakufuata mambo yao, waliisaidia serikali ile lakini hawakuabudu miungu ya watu wa nchi ile, walijihatarisha maisha yao kwa kumwambia mfalme hawawezi kusujudu mungu wake wapo tayari kufa kama Mungu asipowaokoa japo mfalme aliwaandalia moto mara saba zaidi lakini Mungu aliwaokoa kwenye moto.

Leo hii Mungu hatendi kazi duniani sababu watu hawatendi,unatakiwa ufahamu kuwa ukisema wewe ni Mungu amesema, Ukikemea wewe ni Mungu amekemea, Ukigoma wewe Mungu amegoma, ukifyatua wewe ni Mungu amefyatua usikae kimya na kuogopa maana unamfungia Mungu asitende kazi.
Kuna watumishi wanako mtumikia Mungu kwa uaminifu ambao hawaendi mbinguni, kuna watumishi wa Mungu wanaomtumikia Mungu kwa ujanja lakini watakwenda motoni na kuna wale ambao wanamtumikia Mungu lakini hawawezi kwenda mbinguni mfano (kunguru aliyemtumikia Eliya, Punda aliyemsemesha baalam na punda aliyembeba Yesu (mawe nayo yanaweza kumtumikia Mungu na hayawezi kwenda binguni) KILA KITU NI MTUMISHI WA MUNGU.

Kulikuwa na mkono ulioandika ukutani ambapo Danieli aliitwa akatoa tafasiri yake akapandishwa akawa makamo wa Raisi. Waliitwa wachawi kutoa ufumbuzi wa andiko lile na kusema mafumbo yale na Mfalme alitoa ofa ya atakayetoa maana yake atapandishwa mpaka nafasi ya tatu ya juu serikalini, Danieli alifanikiwa kupanda mpaka kwenye nafasi ya juu.

Danieli 6: 8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.”

Daniel 5: 7 Mfalme akalia kwa sauti kubwa, akaamuru waletwe wachawi, na Wakaldayo na wanajimu. Mfalme akanena, akawaambia wenye hekima wa Babeli, mtu awaye yote atakayesoma maandiko haya, na kunionyesha tafsiri yake, atavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu wa tatu katika ufalme. Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.”

Yoshua alikuwa mpelelezi na alimtumikia Mungu, Upelelezi umeanzia kwenye Biblia. leo tuna kitabu cha Yoshua na huyu ndiye aliyewaongoza wana wa Israel kufika nchi ya ahadi.

Hesabu 13: 1 “Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia,Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao. Hayo ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua.”

Esta naye alikuwa mke wa Mfalme lakini alimtumikia Bwana, Alipatwa na jaribio la kwanza la kuifuta Israeli na aliweza kulishinda na hata leo hii ukienda kwenye kumbukumbu za wayahudi kuiangusha Israeli Jaribio hili lililompata Esta utakuta ni la kwanza. Esta aliolewa lakini alimtumikia Bwana kuokoa Israeli isiangamizwe.
Luka 8: 1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.”

Huyu alikuwa ni mwanasheria mkuu lakini alimtumikia Bwana lakini hakuacha taaluma yake alikuwa anamtumikia Bwana huku akifanya kazi yake.

Matendo ya mitume 16: 14 “Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo. Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatushurutisha.”

Mwanamke huyu ndiye aliyewakaribisha wakina Paulo wakakaa nyumbani kwake, ndiye aliyeanzisha kanisa la wafilipi alikuwa anafanya kazi yake na kumtumikia Bwana.

Yeremia alikuwa ni nabii ambaye hajui kusoma wala kuandika ila Mungu alimpa baruku aliyekuwa mwandishi wake ambaye alijua kusoma na kuandika. Baruku alimtumikia Mungu kwa uandishi japo hawa anahubiri. Ukiwa mtumishi wa Mungu mahakamani, au wizarani au sehemu yeyote ile Mungu atakutumia palepale.

Kutoka 1: 15 “Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.”

Wakunga hawa walisema hivyo sababu walikuwa wanamcha Mungu na kumtumikia.

Matendo ya mitume 18: 1 “Baada ya mambo hayo, Paulo akatoka Athene akafika Korintho. Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akila, mzalia wa Ponto; naye amekuja kutoka nchi ya Italia siku za karibu, pamoja na Prisila mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi, naye akafikilia kwao; na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.”

Mtume Paulo alikuwa anamtumikia Mungu na alifanya kazi ya Mungu sana kwasababu alikuwa ana kampuni yake ya kushona mahema na alikuwa anahela ya kusafiria sehemu mbalimbali kuhubiri Injili ya Yesu. Aliweza kuanzisha makanisa na akafanikiwa sana.

Mwanzo 34: 10 “Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.”
Faida za kumtumikia Bwana.

Kutoka 23: 25 “Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.”
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.