SOMO: UNDANI WA MAOMBI (12) - MCHUNGAJI MADUMLA

Watu jamii ya kimasai wakiwa katika maombi ©paulinemaria
Soma sehemu iliyopita kwa Kubonyeza Hapa

04.NI JINSI GANI YA KUOMBA IPASAVYO?

Ukweli ni kwamba sote hatujui kuomba ipasavyo isipokuwa Roho hutusaidia udhaifu wetu (Warumi 8:26). Hivyo basi hakuna mtu anaweza kusema kwamba yeye ni mtaalumu wa maombi au fundi wa maombi pasipo kuwezeshwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu ndio hutuwezesha kuomba ipasavyo,hatuna budi kumjua na kujifunza habari zake kwa usahihi.

Tatizo kubwa linalotukwamisha katika maombi yetu,ni kwamba wengi si wasomaji wa neno la Mungu. Sasa,ikiwa wewe si msomaji na huna neno la Mungu ndani yako; basi ujue hutaweza kuomba ipasavyo,kwa maana itafika wakati hutakosa maneno ya kutamka. Neno la Mungu ni muhimu sana lijae ndani yako katika hekima yote,kusudi likuwezeshe kukupa maarifa katika maombi yako.

Laiti kama tungelikuwa tunamtumia ipasavyo Roho mtakatifu katika maombi yetu,basi ni dhahiri tungelikuwa tuna majibu katika yale tuyaombayo. Hatua zifuatazo zinafaa sana pale unapoingia katika maombi ya aina yoyote ile(Lakini sio kanuni bali ni vyema sana ukatumia hatua hizi uombapo). Hivyo basi zipo hatua tatu muhimu sana katika maombi yako,nazo ni;

i) Kushukuru~ Kabla hujaanza kuomba ombi lako,basi ni vyema ukaanza kumshukuru Bwana Mungu wako kwa mema aliyokutendea na anayokutendea kila saa,kila siku. Kila mtu,ametendewa na Mungu kwa maana hata pumzi tu ile tunayoivuta,yatosha kumshukuru Mungu.

“ Haleluya.Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,Kwa maana fadhili zake ni za milele.” Zab.106

ii) Toba na rehema.~ Tunatambua ya kwamba tu wakosefu mbele za Mungu,hivyo hata kama tumeokoka hatupaswi kujihesabia haki kiasi cha kushindwa kutubu kwa maana zipo dhambi zinazotuzinga kwa wepesi, (Waebrania 12:1).

Wapo baadhi ya wapendwa wameisukumia mbali imani ya toba,wakidai kwamba hakuna haja ya kutubu mara kwa mara maana toba walioifanya siku ya kuokoka kwao inatosha.Watu wa namna hii wanajidanganya nafsini mwao,kwa maana ikumbukwe kwamba ingawa tupo rohoni lakini pia tunaishi mwilini,ambapo asili ya mwili ni dhambi;

kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho,hizi zimepingana (Wagalatia 5:17).Hivyo ni vyema ukifanya maombi yako ukawa na muda wa kuomba rehema za Mungu. Ukatubie maovu yako yote,kisha ndipo uendelee. Tazama tena,inawezekana ukawa unaomba uponyaji juu yako au juu ya mwingine.

Lakini ukawa huoni mpenyo wa uponyaji kwa sababu ya uwepo wa dhambi,kwa sababu chanzo cha magonjwa mengi ni dhambi ndani ya mtu.Ndiomaana mtunga Zaburi amesema “ Akusamehe maovu yako yote,Akuponya magonjwa yako yote,” Zab.103:3, ;

hii ikiwa na maana kwamba unaposamehewa dhambi zako basi ujue uponyaji ni mali yako. Hata unapoenda kumuombea mtu,hakikisha unamuongoza sala ya toba,mtubishe vizuri ili uponyaji uanze kuumbika.

iii)Kuomba msaada wa Roho mtakatifu.~ Ni muhimu ukaomba msaada wa Roho mtakatifu ili akusaidie kuomba ipasavyo. Akupe wepesi wa maombi yako na akuwezeshe kwenye kila eneo. Hapo sasa waweza kuendelea na maombi yako uliyopanga.

Inawezekana ukawa unafanya maombi bila kuyazingatia haya,kisha ukaona kama vile umekwama kimaombi. Au inawezekana ukawa unazijiua hatua hizi,lakini hujui unaanzaje na unamalizaje. Ninaomba niombe na wewe leo,nipigie kwa namba zilizopo hapo chini;

ITAENDELEA…

Kwa huduma ya maombezi,piga +255655 111 149,+255 684 033 334.

Mch.G.Madumla

Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.