TAREHE 7 AGOSTI NI ZAMU YA MESS JACOB CHENGULA MITO YA BARAKA

Mess kwenye mojawapo ya tamasha la pasaka.
Kuanzia mwaka 2012 Mess Jacob Chengula ameshika hatamu kuhubiri Injili kwa njia ya uimbaji, na kati ya nyimbo zake maarufu ni pamoja na Mungu Habadiliki ambao umebeba jina la albamu yake ya kwanza. Hivi sasa tunazungumzia kuhusu albamu ya pili - Moyo Wangu Hauna Uoga.

Mkondo ambao Mess ameuchukua kwa awamu hii ni kufanya huduma hii kwa ubora zaidi ili mataifa yote kuanzia Tanzania na hata Afrika Mashariki yote pamoja na ulimwengu kupata shauku ya kutazama kazi yake.

Wimbo huu unaobeba jina la album umeimbwa kwa kushirikiana na mwanamama Upendo Nkone, na kama hufafamu, basi ni kwamba Upendo Nkone ni role model wa Mess. Kwa lugha yetu ni kwamba ndiye anayempa hamasa ya kufanya vizuri zaidi kwenye tasnia hii ya muziki wa injili.

Fuatilia mahojiano haya kupitia GK TV kama ambavyo Silas Mbise amemuhoji Mess, kazi ambayo imeandaliwa na Bony Kazi.


Tukutane Jumapili kanisa la EAGT Mito ya Baraka kuanzia saa nane mchana.Team GK itakuwepo.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.