TUNACHAGUA KUMSIFU MUNGU NA WAFUNGWA WA JELA YA NAIVASHA

Sehemu ya waimbaji wa kwaya hiyo ya jela ya ulinzi mkali ya Naivasha

Tunatumai u mzima mdau wa Gospel Kitaa. kwa Jumapili ya leo ambayo inatufikisha karibu ya mwezi huu wa nane, tunakuletea chaguo kutoka jela yenye ulinzi mkali ya Naivasha.

Kama wewe hujapata sababu ya kumsifu Mungu, basi wenzako wameamua kumsifu Mungu kutokea huko waliko. Popote ulipo unaweza kulisifu Jina la Yesu kwa makubwa na magumu aliyokufanyia.

Mipango na Misri ndio nyimbo ambazo tunakuletea kutoka kwaya hii ya "Naivasha Maximum Security Prison Inmate SDA Choir".

Wimbo wa Mipango unaeleza namna ambavyo mpango wa Mungu ulivyo juu ya mwanadamu, kuanzia kuasi kwa shetani hata kuja kwa Yesu kuokoa wataoamini. Wimbo wa Misri unaeleza namna ambavyo wameteseka na dhambi Misri hadi Mungu akawaokoa na sasa wanaishi kwa raha Kaanani.Tunatumai uimbaji huu wa wafungwa pamoja na walinzi wa huko gerezani utakugusa na kubadili kitu ndani yako kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.